Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanafunzi wapigwa marufuku mavazi ya ‘Squid Game’
Kimataifa

Wanafunzi wapigwa marufuku mavazi ya ‘Squid Game’

Spread the love

 

SHULE tatu za msingi katika jimbo la New York nchini Marekani zimepiga marufuku mavazi ya ‘Halloween’ yanayofanana na yale yaliyovaliwa na washiriki wa tamthilia maarufu ya Netflix, Squid Game, kwa kuhofia kwamba yanaweza kuchochea vurugu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tamthilia hiyo ya kusisimua ya Korea Kusini inaeleza kuhusu hadithi ya watu wazima wanaoshindania zawadi ya pesa kwa kucheza michezo ya watoto, na ambao wako tayari kuhatarisha maisha yao ili kushinda.

Maudhui yake yanayoonekana kwenda kinyume na maadili kwa baadhi ya jamii yamesababisha shule kuwatumia barua pepe wazazi kuhusu ujumbe wa uchochezi uliomo kwenye tamthilia hiyo.

Shule hizo zimesema mavazi ya mchezo wa Squid katika hafla za shule hayatafaa.

Mkuu wa Shule ya Fayetteville ya New York, Dk. Craig Tice amesema muongozo wa shule hiyo umepiga marufuku mavazi ya Halloween yenye vitu vinavyoweza kufasiriwa kama silaha na vya kutisha.

Nchini Marekani, tamthilia hiyo imewekwa na mtandao wa Netflix kwenye darala la kuangaliwa na hadhira ya watu wazima hii ikimaanisha kwamba tammthili hiyo haitakiwi kutazamwa na watoto chini ya umri wa miaka 17.

Aidha, baadhi ya wazazi wanaripotiwa kutofurahishwa na marufuku hiyo ya mavazi iliyotolewa na shule hizo.

“Ni vazi tu. Jambo la msingi ni kutoruhusu watoto wako kutazama tamthilia hiyo,” amesema mwanamke mmoja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!