Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba ajitosa sakata la mauaji Palestina
Habari za Siasa

Prof. Lipumba ajitosa sakata la mauaji Palestina

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amepanga kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na waumini wa kiislam dhehebu la Shia, kwa ajili ya kupinga mauaji yanayoendelea katika ukanda wa Gaza. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na  Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma CUF, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, maandamano hayo yamepangwa kufanyika kesho Ijumaa, tarehe 5 Aprili 2024, maeneo ya Ilala jijini Dar es Salaam.

 

Kupitia taarifa hiyo, Mhandisi Ngulangwa amewataka wanachama wa CUF kujitokeza kushiriki maandamano hayo.

“Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Julius  Nyerere aliliachia taifa heshima kubwa kwa kutetea wanyonge na kupinga dhulma kokote duniani. Kuhusu mgogoro ukanda wa Gaza, Msimamo wa Tanzania ulikuwa ni kusimama upande wa utetezi wa haki ya Wapalestina, wanaoteswa katika ardhi yao,” imesema taarifa ya Mhandisi Ngulangwa na kuongeza:

“Katika kuenzi msimamo wa Mwalimu Nyerere, Prof.  Lipumba atashiriki kwenye maandamano yanayoandaliwa na waislam wa kishia yaliyopangwa kuanza Ilala Boma kuanzia saa 2:00 asubuhi. Mashia duniani huitumia Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kila mwaka kuadhimisha siku ya mshikamano na Wapalestina (Maarufu kwa jina la QUDUS).”

Mauaji hayo yanatokana na vita inayoendelea ndani ya ukanda huo ambayo imedumu kwa miezi sita, tangu kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas, kufanya shambulizi la kushtukiza upande wa Israel mnamo Oktoba 2023 na kuuawa watu zaidi ya 1,000.

Kundi la Hamas na Serikali ya Israel wamekuwa katika mvutano unaosababishwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu, ambapo kundi hilo lindaiwa kufanya tukio hilo likishinikiza waisrael kuwaachia maeneo yao wanayodai wanakaa kimabavu.

Kufuatia shambulizi hilo la kushtukiza, Serikali ya Israel iliamua kujibu mapigo kwa kuanzisha mapigano yanayoendelea mfululizo, ambapo wapalestina ni wahanga wakuu wa vita hiyo kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha, kujeruhiwa na hata makazi yao kubomolewa.

Kwa mujibu wa ripoti za jumuiya za kimataifa, hadi kufikia Machi 2024, wapalestina 30,228 wamefariki katika mapigano hayo, wakati kwa upande wa Israel waliopoteza maisha ni 1,410.

Jumuiya za kimataifa zimetoa wito kwa Serikali ya Israel kusitisha mapigano hayo, bila mafanikio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!