Monday , 29 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wazuia mkutano wa ACT-Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

Polisi wazuia mkutano wa ACT-Wazalendo

Spread the love
JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam, limepiga marufuku mkutano wa kisiasa wa Chama cha ACT-Wazalendo, kwa madai ya kuwapo tishio la vurugu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa chama hicho zinasema, polisi wamezuia mkutano huo kwa maelezo kuwa wamepata taarifa za “kiteljensia,” zinazoonyesha kuwa kundi linalomuunga mkono Prof. Ibrahim Lipumba, limepanga kuvuruga mkutano huo.

Amesema, “ni kweli kwamba mkutano wetu umezuiwa na jeshi la polisi. Wanadai kuwa wamepata taarifa zinazoonyesha kuwa genge la Lipumba limepanga kufanya vurugu.”

Haya yanatokea, siku mbili baada ya ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kukiandikia barua chama hicho kutaka kijieleza kwa nini kisifutiwe usajili wake kutokana na kinachodaiwa kushindwa kuwasilisha ripoti ya hesabu zake kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Katika barua yake kwa katibu mkuu wa ACT – Wazalendo, yenye Kumb. Na. HA. 322/362/20/98, Msajili anakituhumu chama hicho kukiuka sheria ya vyama vya siasa kwa kutopeleka kwake, hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

Barua ya Msajili kwenda ACT na ambayo imesheheni tuhuma hizo, iliandikwa tarehe 25 Machi 2019.

Aidha, msajili anataja sababu nyingine ya kutaka kufuta ACT, ni “kuchomwa moto bendera na kadi za Chama cha Wananchi (CUF) na matumizi ya neno takbira lililotumika kwenye baadhi ya shughuli zake.”

Mkutano wa ACT- Wazalendo ambao umezuiwa na polisi, ulilenga kukitangaza chama hicho jijini Dar es Salaam. ACT kimeanza kuwa moja ya vyama tishio nchini, kufuatia hatua ya aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na baadhi ya viongozi wenzake, kuamua kuondoka CUF na kujiunga na chama hicho.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa mkutano wa jijini Dar es Salaam, utaongozwa na Zitto Zuber Kabwe, kiongozi mkuu wa chama hicho; Maalim Seif na naibu kiongozi wake mkuu, Juma Duni Haji.

Mkutano utafanyika katika ukumbi wa PR Stadium uliyo karibu na uwanja wa mpira wa taifa wa zamani – Shamba la Bibi – kuanzia saa nne asubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

error: Content is protected !!