Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Waziri Mkuu atoa onyo kwa maofisa Elimu
Elimu

Waziri Mkuu atoa onyo kwa maofisa Elimu

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa onyo kwa maofisa elimu nchini kutojihusisha kwenye vitendo vya kupanga na kuiba mitihani ya kitaifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Amesisitiza kuwa serikali haitomsamehe yeyote atakayebainika kwenye wizi huo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo jana jijini hapa wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Umoja wa Maofia Elimu Mkoa na Wilaya.

“Kumekuwepo na walimu wanaoshirikiana na Maofisa Elimu kuiba mitihani. Ninatoa onyo kali kwa baadhi yenu wanaojihusisha na wizi, udanganyifu na uvujaji mitihani.

“Tabia na mwenendo huu unalivunjia heshima na hadhi taifa letu,” alisisitiza.

Waziri Mkuu aliziagiza kamati za mitihani za mikoa na wilaya kusimamia sheria, kanuni na taratibu bila uwoga, upendeleo na kutoyumbishwa.

Alisema hatua kali za kinidhamu na kiutumishi zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukiuka sheria, taratibu na miongozo inayotolewa.

Kadhalika, Majaliwa aliwataka maofisa elimu nchini kusimamia nidhamu na mienendo ya wanafunzi.

“Tatizo la nidhamu mbaya kwa wanafunzi ni jukumu la walimu wote wanatakiwa kutekeleza majukumu yao ya kufundisha, kulewa, kuwaongoza na kuwaendeleza wanafunzi kimwili.

“Serikali imesikitishwa na matukio ya hivi karibuni ya athari ya viboko kwa wanafunzi shuleni ikiwemo kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu pamoja na tukio la kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius wa Shule ya Msingi Kibeta,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa (CCM), alisema kuna udhaifu katika utaratibu wa utoaji na usimamizi wa adhabu ya viboko shuleni.

Aliwakumbusha maofisa elimu kuwakumbusha walimu kuzingatia mwongozo wa kutoa adhabu shuleni chini ya kifungu cha 61 cha Sheria ya Elimu sura 353 pamoja na kanuni zake.

Pia aliwaagiza maofisa elimu kutokaa maofisini wakati walimu wapya wanaporipoti shuleni bali wanapaswa kukawekea motisha ikiwemo kuwapeleka na magari ya halmashari kwenye vituo vyao vya kazi.

“Mfano mzuri ni Mkoa wa Njombe ambapo mwalimu akiripoti anapatiwa kitanda, godoro, gunia la mahindi, viazi na maharage. Kwa kufanya hivyo kunamfanya mwalimu ajione yupo nyumbani na hatoweza kuondoka,” alieleza.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, alisema wizara yake pamoja na TAMISEMI zimekuwa zikifanyakazi kwa karibu zaidi katika kutatua changamoto mbalimbali Za kitaalamu na kitaaluma.

Pia aliwataka maofisa elimu kutoa taarifa na takwimu sahihi kuhusu elimu ili ziweze kutumika kwenye mipango mbalimbali ya elimu badala ya kuzipika.

Naye, Waziri wa Nchi TAMISEMI, Seleman Jafo, aliwaagiza maofisa elimu kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!