Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wapata maarifa na mbinu ukatili wa kijinsia kutoka Tengeru
Habari Mchanganyiko

Polisi wapata maarifa na mbinu ukatili wa kijinsia kutoka Tengeru

Spread the love

 

JESHI la Polisi kupitia Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kimeendelea kupata elimu na maarifa kutoka kwa vyuo mbalimbali ndani nan je ya Nchi ambapo Taasisi ya Maendeleo ya jamii Tengeru wametoa Elimu na mafunzo ya ukatili wa kijinsia katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam lengo likiwa ni kuwapa maarifa mapya kukabiliana na matukio hayo. Anaripoti Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es Salaam … (endelea).

Mwezesha wa mafunzo hayo Everlyne Rwela ambaye ni Mkuu wa idara ya Jinsia kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru amesema kuwa wametoa mafunzo kwa askari wa Jeshi la Polisi ambao ni wahusika wakubwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto ambapo amebainisha kuwa wamefundisha maswala ya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha kitaifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho yanayohusu wanawake kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Bi Rose Mtei amesema kuwa waliona vyema kama taasisi watoe elimu ya ushirikishwaji jamii kwa mifano ambapo amebainisha kuwa wataendele kuwekeza katika kufundisha wa ushirikishwaji katika jamii ili kuwaongezea maarifa Jeshi hilo.

Nae Mkuu wa kitengo cha utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam amesema Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Ralph Meela amebainisha kuwa kuwa maafisa hao wanafunzi wanakwenda kutoa huduma bora Zaidi kutokana na elimu na maarifa hayo mapya waliopata kutoka katika tasisi hiyo yanakwenda kujibu changamoto za ukatili katika jamii ya watanzania.

Sambamba na hilo Mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Artidius Ryabugaba hamesema kuwa kutokana na elimu hiyo imewaongezea maarifa katika kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Pia mkaguzi msadizi mwanafunzi Kangale Makweta amesema yuko tayari baada ya mafunzo yake katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kwenda kuhudumia wananchi baada ya kupaata mbini za kukabiliana na vitendo vya ukatili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!