Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya NBC yaungana na Taasisi ya Benjamini Mkapa kusomesha wakunga 100
Afya

NBC yaungana na Taasisi ya Benjamini Mkapa kusomesha wakunga 100

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na Taasisi ya Benjamini Mkapa kuanzisha mpango wa kutoa ufadhili wa masomo (scholaships) kwa wanafuzi wa taaluma ya ukunga nchini ili kuunga mkono juhudi za kupambana na changamoto za vifo vinavyotokana na uzazi kwa akina mama. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia wakina mama wajawazito, jambo ambalo husababisha kutokea kwa vifo vingi vinavyoweza kuepukika.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (aliyekaa kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dk. Ellen Mkondya (aliyekaa kushoto) wakitia saini makataba wa makubaliano baina ya taasisi hizo mbili ambapo Benki ya NBC itatoa kaisi cha Sh 200 milioni kusomesha wakunga 100 katika kpindi cha miaka miwili ikiwa ni mchango wake katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2020, karibu asilimia 95 ya vifo vya akina mama wajawazito vilitokea katika nchi zinazoendelea huku idadi ya vifo hivyo kwa Tanzania ikiwa juu.
Hayo yanajiri huku kukiwa na jitihada mbalimbali zinazofanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya afya, kuongeza watumishi wenye ujuzi na nyinginezo.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini ushirikiano huo leo tarehe 4 Julai 2023, Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NBC, Theobald Sabi amesema benki ya NBC inayofuraha kutoa mchango wake katika kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
Amesema ushirikiano kati ya benki ya NBC na Taasisi ya Benjamini Mkapa ni wito wa wadau kuungana katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Amesema kupitia ushirikiano huo, NBC itatoa ufadhili wa masomo kwa wakunga na hivyo kuboresha huduma kwa wajawazito lengo likiwa ni kupunguza vifo vinavyoepukika.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dk. Ellen Mkondya wakionyesha mkataba waliosaini kusaidia mapambano dhidi ya vifo vinavyotokana na uzazi hapa nchini.

“Tukiwa kama benki inayothamini ustawi wa jamii tunajivunia kutoa mchango wetu kusaidia maendeleo ya jamii ambayo tunaihudumia. Tunafahamu umuhimu na uharaka wa kushughulikia suala la vifo vinavyotokana na uzazi hapa nchini na tunaamini uwekezaji kwenye elimu na mafunzo kwa wakunga wetu kutasaidia sana kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Theobald Sabi (wanne kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dk. Ellen Mkondya (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hizo mbili muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa kusaidia afya ya akina mama wajawazito.

“Ni furaha kwetu kutoa sehemu ya kiasi kinachopatikana kutokana na uchangishaji fedha wetu wa kila mwaka kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon na kuzielekeza kwenye utatuzi wa chagamoto hii,” amesema.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dk. Ellen Mkondya ameishukuru benki ya NBC na kuwataka wadau wengine kufuata mfano wa benki hiyo ili kuongeza nguvu katika kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.
“Tunayofuraha kushirikiana na benki ya NBC katika lengo letu kuu la kupambana na vifo vya wajawazito hapa nchini. Ufadhili wa masomo unaotolewa na benki ya NBC utasaidia kuboresha ujuzi wa wakunga wetu na hivyo kuboresha huduma za uzazi salama,,” amesema.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Dk. Ellen Mkondya akiwa anatia sahihi katika bango la ushiriki wa mbio za NBC Dodoma Marathon muda mfupi baada ya taasisi hizo mbili kutia saini mkataba wa kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi. Anayetizama kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Theobald Sabi.

Kupitia ushirikiano huo wa miaka miwili, NBC itatoa kiasi cha Sh.200 milioni ambazo zitatumika kusomesha wakunga 100 katika kipindi husika na hivyo kusaidia kuongeza nguvu kazi yenye ujuzi katika kuwahudia akina mama wajawazito.

Benki ya NBC na taasisi ya Benjamini Mkapa zinaamini kuwa uwekezaji katika elimu na mafunzo kwa  wakunga ni hatua muhimu katika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo endelevu namba 3 ambalo linalenga kusaidia ustawi kwa wote ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!