FOMU za kuwania ubunge na udiwani katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 202 zinaanza kutolewa leo Jumatano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaonyesha, shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu itaanza leo Jumatano tarehe 12 hadi 25 Agosti 2020.
Fomu za ubunge zitatolewa Ofisi za Halmashauri huku za udiwani zikitoleaa Ofisi za Kata.
Tayari fomu za kuwania kuteuliwa kugombea urais zimeanza kutolewa tangu tarehe 5 Agosti 2020 ofisi za NEC Ndejegwa jijini Dodoma.
Hadi jana Jumanne, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk. Charles Mahera alisema vyama 16 kati ya 19 vyenye usajili wa kudumu vilikuwa vimechukua fomu.
Tarehe 25 Agosti 2020 ambayo ni siku ya mwisho kuchukua na kurejesha ndiyo siku ya uteuzi wa wagombea na 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020 na kesho yake ndiyo itakuwa ni siku ya upigaji kura.
Baadhi ya vyama vimekwisha kuteua wagombea ubunge katika uchaguzi huo, miongoni ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kati ya majimbo 264 ya uchaguzi kwa maana ya 214 ya Tanzania Bara na 50 Zanzibar, Chadema imeteua wagombea kwenye majimbo 163 na mengine bado inaendelea.
Chama tawala cha Mapinduzi (CCM), chenyewe bado hakijafanya uteuzi wa wagombea wake.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jumla wa wananchi milioni 29 wamejiandikisha kupiga kura na vituo vya upigajikura vitakuwa 80,155.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarif mbalimbali.
Leave a comment