December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Paredi ya ng’ombe kufanyika kesho

Spread the love

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdalah Ulega anatarajiw kuwa mgeni Rasm kesho saa mbili na nusu kwenye maonesho ya gwaride la ng’ombe bora nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Maonesho hayo ambayo yanafanyika kitaifa jijini Dodoma katika viwanja vya maonesho ya Nanenane yanalenga kuongeza hamasa katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa Maziwa. 

Akizungumzia maonesho hayo, Katibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa Tanzania ni kati ya nchi zenye ng’ombe wengi hivyo kuna haja ya kuboresha mifugo hiyo.

Katibu huyo amesema kuwa maandalizi ya maonesho hayo yanayofanyika kitaifa na kwa mara ya kwanza ni kutia amasa ya kuwafanya watanzania kuacha kujifuna kuwa na wingi wa mifugo bali wawe na mifugo ambayo ina uzito mkubwa.

error: Content is protected !!