Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Malalamiko ya kupikwa takwimu: Upinzani waitaja IMF
Habari za Siasa

Malalamiko ya kupikwa takwimu: Upinzani waitaja IMF

David Silinde, Naibu Waziri TAMISEMI
Spread the love

KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kwamba, kuna kila sababu ya kukwepa kupika takwimu ili kuepuka kujenga uchumi hewa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17 Juni 2019, na David Silinde, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Uchumi wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo bungeni, jijini Dodoma kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/20.

Akiwasilisha maoni hayo Silinde amesema, takwimu hizo zenye mashaka zimekuwa zikipingwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na kwamba, ipo haja ya kuchunguza uhalisia wake.

“Ipo haja ya kuchunguza uhalisia wa takwimu zetu, kuepuka kujenga uchumi hewa kwa takwimu za kupika. Ndio sababu IMF ilitoa angalizo kwa mwaka wa fedha 2018/19 kwamba; mwenendo mbovu wa sera za kibajeti na kutokutabirika kwa utawala huu kutasababisha kuzorota kwa uchumi,” amesema Silinde.

Amesema, kumekuwa na changamoto kubwa hata kwa miongoni mwa wachumi kuhusu hali ya uchumi nchini hasa inapoonekana biashara nyingi zinafungwa kwa kushindwa kujiendesha, kusinyaa kwa uwekezaji mkubwa, kuyumba kwa biashara katika sekta ya nyumba (real estate), kampuni mbalimbali kupunguza wafanyakazi, kuporomoka kwa thamani ya hisa katika soko la mitaji, ukata kwenye uchumi.

“Mwenendo mbovu wa sera za kibajeti na kutokutabirika kwa utawala huu, kutasababisha kuzorota kwa uchumi.

Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya saba ya hali ya uchumi wa Tanzania iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) tarehe (11/01/2018) – takribab  mwaka mmoja na nusu uliopita;  ni kwamba hali ya uchumi wa Tanzania imekuwa ikipanda na kushuka na kwamba, matazamio ya mwenendo huo yanaonyesha mashaka,” Silinde amenukuu kwenye maoni hayo.

Amesema, ujazo wa fedha Benki Kuu umeshuka na kusababisha kushuka kwa kiwango cha mikopo kutoka Benki za biashara kwa sekta binafsi, na hivyo kuyumba kwa sekta binafsi ambayo kimsingi ndio injini ya uchumi.

“Na ndio sababu Benk Kuu ya Tanzania, kama msimamizi wa sera ya fedha, ikachukua hatua mbili kama namna ya kutafuta ufumbuzi wa ukata wa fedha kwenye uchumi (liquidity tightness).

“Hatua ya kwanza ni ile ya tangazo la kupunguza riba kwa mikopo ya Bank kuu kwenda bank za  biashara kutoka riba ya asilimia 16 mpaka riba ya silimia 12. Ikafuatiwa na tangazo la Benki Kuu la kupunguza dhamana za Benki za biashara zinazowekwa benki kuu kutoka asilimia 10 mpaka asilimia 8,” amesema.

 Amesema, tatizo  la uchumi kwasasa sio benki kukosa fedha kukopesha sekta binafsi, tatizo ni serikali imeshindwa kujenga mazingira rafiki kwa biashara na wawekezaji kwa ujumla.

Kwenye maoni hayo Silinde amesema, wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje  kwa ujumla wanakabiliwa na mazingira magumu kibiashara, na ndio sababu kiwango cha mikopo isiyolipika kimezidi kuongezeka kwa kiasi ambayo hakijawahi kutokea kwa zaidi ya miongo miwili.

Amesema, kwa mujibu wa ripoti ya BoT, kiwango cha mikopo isiyolipika kimefikia zaidi ya asilimia 10 ambapo wastani ni asilimia 5.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!