July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge Chadema, CCM walichoka gazeti la Tanzanite

Hussein Bashe, Mbunge wa Nzenga Vijijini (kulia) na Cecil Mwambe, Mbunge wa Ndanda (Chadema)

Spread the love

MBUNGE wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema) na Mbunge wa Nzega Vijijini, Hussein Bashe wamehoji jeuri ya gazeti la Tanzanite kuwatukana watu inaipata wapi? Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wabunge hao wameliita gazeti hilo kuwa la kihuni na lisilo na maadili kwamba, limekuwa likiwatuhumu baadhi ya watumishi mabalimbali, huku serikali ikibariki kwa kutoa matangazo katika gazeti hilo.

Cecil amedai, imekuwa ni kawaida kwa gazeti hilo kutumiwa na serikali na limekuwa likiwachafua watu bila kuchukuliwa hatua yoyote. 

Amedai kuwa, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na CCM, imekuwa ikitumia gazeti hilo kuwapa matangazo licha ya nakala za gazeti hilo kutofika hata 2000.

Naye Bashe akitoa taarifa kwa Mwambe amesema, anachoamini kwamba CCM ni chama makini hivyo hakiwezi kutumia gazeti la kihuni tena lisilo na maadili kwasababu, limekaa kihuni.

Katika hatua nyingine ametaka kujua kama Rais John Magufuli amekuwa na lengo la kutoa vitambulisho kwa wajasiliamali au kuwauzia.

error: Content is protected !!