Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Oryx Gas, ASAS wawafuta machozi waathiriwa mafuriko Rufiji
Habari Mchanganyiko

Oryx Gas, ASAS wawafuta machozi waathiriwa mafuriko Rufiji

Spread the love

KAMPUNI ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Kampuni ya ASAS wamekabidhi msaada wa vyakula pamoja na mitungi ya gesi ya Oryx kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Msaada huo umekabidhiwa leo tarehe 13 Aprili 2024 jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa kuwasaidia wananchi wilayani humo waliopatwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza wakati akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi, Waziri Mchengerwa amezishukuru kampuni hizo kwa kuguswa na janga hilo na kujitolea kuwaunga mkongo wana Rufiji kutokana na changamoto iliyowakumba.

“Niko hapa kwa ajili ya kupokea msaada kama tunavyofahamu hali ya Rufiji kila mmoja wenu anatambua kwamba mwaka huu mafuriko yamekuwa makubwa kupita kiasi, tunayafananisha mafuriko ya mwaka huu na mafuriko yaliyotokea mwaka 1972 na mwaka 1974.

“Ambapo Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) alilazimika yeye na Makamu wa Pili wa Rais wakati huo mzee Rashid Mfaume Kawawa kwenda Rufiji wao kwa pamoja kuzunguka na kutoa pole kwa wananchi.

“Leo tunaashuhudia kwa mwamko wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye yeye ni mfariji namba moja katika taifa letu alioutoa kwa siku ya jana alipokuwa kule Arusha lakini taarifa ambazo amekuwa akizitoa kuwataka Watanzania kuwa wamoja na kusaidia wale ambao wana nafasi basi wajitolee kwa ajili ya wenzao,”amesema huku akiendelea kuwashukuru Oryx na ASAS KWA msaada huo.

Awali kabla ya kukabidhi msaada huo, Meneja Mauzo wa Oryx Gas Shaban Fundi  amesema kwa niaba ya  Oryx Energies wanatoa pole kwa waathirika wote wa mafuriko yaliyotokea nchini hususan watu wa Rufiji.

“Kampuni ya Oryx Gas ikishirikiana na wadau wenzetu ASAS tumeamua tuwashike mkono wenzetu wa Rufiji kwa kuwapa msaada wa vyakula na mitungi ya gas ili kusaidia watu waliopo katika makambi ya kutolea misaada ya kibinaadam.

“Tumetoa mchele, unga wa sembe, mafuta ya kupikia yenye thamani ya zaidi ya milioni 52. Zaidi tumetoa mitungi mikunwa 100 na majiko 100, pia tumetoa mitungi midogo 100 yenye thamani ya zaidi ya mili 25.Tunampa pole muheshimiwa Waziri Mchengerwa, Wananchi wa Rufiji na Serikali kwa ujumla,”amesema Fundi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!