Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yatenga bilioni 1 kuwawezesha wabunifu wanaochipukia
Habari Mchanganyiko

NMB yatenga bilioni 1 kuwawezesha wabunifu wanaochipukia

Spread the love

BENKI ya NMB imeendelea kuunga mkono juhudi ya Serikali kupitia Wizara ya Sayansi, Elimu na Teknolojia, kwa kutenga kiasi cha bilioni moja kwa ajili ya kuwasaidia wabunifu wanaochipukia kuziweka bunifu zao katika utekelezaji ili waweze kunufaika.

Pia imedhamini na kushiriki Wiki ya Ubunifu Tanzania 2023, yenye kauli mbiu ya ‘Ubunifu kwa Uchumi Shindani’ inayofanyika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 27 Aprili 2023 jijini Dodoma na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi wakati akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rose Senyamule  masuluhisho yao ya kidijitali alipotembelea banda la NMB kuhusu katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Amesema kiasi hicho cha Sh bilioni moja sio mkopo bali ni fedha iliyotengwa kwa dhumuni ya kusaidia wabunifu hao na hawatawajibika kuirejesha.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule alipotembelea banda lao kuhusu masuluhisho yao ya kidijitali katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Aidha, amesema ushiriki huo wa NMB katika wiki ya ubunifu, unalengo la kuwawezesha wabunifu kujionea na kujifunza bunifu za kiteknolojia za masuluhisho ya kifedha, na kuweza kujaribu masuluhisho yao kupitia mfumo wa ‘NMB Sandbox environment’.

“Mfumo huo unatoa fursa kwa wabunifu wa masuala ya kifedha kufanya majaribio ya bunifu zao na kisha kuwasaidia wabunifu hao kuingia sokoni.

“NMB ipo kwenye viwanja vya Jamhuri – Dodoma wiki nzima. Tembelea banda lao kujua zaidi kuhusu suluhishi za kidijitali,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!