Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yaendelea kung’ara, yatwaa tuzo ya mwajiri bora Afrika
Habari Mchanganyiko

NMB yaendelea kung’ara, yatwaa tuzo ya mwajiri bora Afrika

Spread the love

KWA mara nyingine tena, Benki ya NMB imedhihirisha umahiri na ukubwa wake kiutendaji na kiundeshaji nchini baada yakufanikiwa kunyakuwa tuzo ya mwajiri bora barani Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ushindi huo mkubwa ulipatikana wiki jana mjini Port Louis huko Maurituis ambako NMB ilitunukiwa tuzo hiyo inayotambua umakini katika kuzingatia maslahi na maendeleo ya wafanyakazi na waandaaji wake ambao ni taasisi ya ajira ya Employer Branding Institute.

Tuzo hii imetolewa kwenye hafla iliyofanyika nchini Mauritius na Afisa Mkuu wetu wa Rasilimali Watu – Emmanuel Akonaay aliipokea kwa niaba ya Nmb na leo tarehe 19 Disemba, 2022 na ameikabidhi rasmi kwa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara – Filbert Mponzi, kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu – wa NMB.

Akipokea nishani hiyo jana, makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Filbert Mponzi, alisema tuzo hiyo ya nne ya mwajiri bora mwaka huu, ni ushahidi mwingine wa jinsi taasisi hiyo kubwa ya fedha nchini inavyothamini wafanyakazi wake.

“Thamani ya wafanyakazi kwetu sisi NMB ni kubwa sana kwani wao ndiyo rasilimali inayoongoza na chanzo cha mafanikio yetu yote na tuzo mbalimbali ambazo tumekuwa tuzazipata,” alisema Mpozi baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Afisa Mkuu Rasilimali Watu Emmanuel Akonaay.

Kiongozi huyo ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB aliongeza kuwa baada ya kuongoza karibu kwa kila kitu nchini, sasa wameanza kupata mafanikio barani Afrika.

Hii inatokana na NMB kuzingatia matakwa ya msingi ya uongozi na uendeshaji taasisi hasa zile za fedha. Ushindi wa mwajiri bora, alifafanua, unatokana na NMB kutambua umuhimu wa rasilimali watu na kuwekeza katika maendeleo yake.

“Rasilimali watu ndiyo mtaji wetu mkubwa na ushindi huu unadhihirisha jinsi tunavyothamini rasilimali hii. Mafanikio haya yanawafanya wafanyakazi wa NMB kujivunia kufanya kazi na mwajiri bora nchini na Afrika,” Bw Mponzi alibainisha kwenye hafla fupi ya kupokea tuzo hiyo ya “the Best Employer Brand – Africa”.

“Maana kubwa ya ushindi huu ni kuwa matokeo na mafanikio yote makubwa ambayo NMB inayapata yanatokana na kuzingaitia maslahi na maendeleo ya wafanyakazi,” aliongeza.

Mbali ya kuwa mwajiri bora, pia NMB ndiyo benki bora na kiongozi nchini. Katika miaka miwili iliyopita pekee, NMB imeweza kujikusanyia zaidi ya tuzo 20 za kimataifa ilizotunukiwa na majarida yanayoheshimika duniani kama vile World Economic Magazine, Global Brands Magazine, International Banker Awards na International Business Magazine.

Kwa mwaka huu, hii ni tuzo ya 21 kupata ndani na nje ya nchi. Mwezi jana, NMB alinyakua tuzo tatu za mwajiri mahiri kukoka kwa chama cha waajiri nchini (ATE) ikiwemo ile ya mwajiri bora wa mwaka 2022.

Jana, Akonaay ambaye ndiye aliipokea tuzo ya Best Employer Brand – Africa huko Mauritius tarehe 13 mwezi huu alisema tuzo hiyo ni mwendelezo wa mambo makubwa ya NMB kwa mwaka huu.

Akizungumza kabla ya kuikabidhi rasmi kwa Mponzi, mtaalamu huyo wa ajira na wafanyakazi alisema heshima waliyopata inazidi kuifanya NMB kutambulika barani Afrika na duniani kote kwa ujumla.

“Mafaniko haya yanafuatia yale yaliyopatikana kutokana na ushindi wa Jasiri Bond na EDGE Certification (cheti maalumu cha kutambulika rasmi duniani kama kinara katika mgawanyo wa kiuchumi kwenye suala la kijinsia)”, Bw Akonaay alisema.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa ushindi walioupata unatokana na juhudi za bodi na manejimenti ya NMB lakini zaidi wafanyakazi wa benki hiyo. NMB, alifafanua, imeonyesha kuwa si tu taasisi inayoongoza kwa huduma za kifedha bali pia ni kinara wa kujali maslahi ya wafanyakazi wake.

“Sisi tunaongoza si tu kwa biashara na huduma bora bali pia linapokuja swala la rasilimali watu,” alieleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!