Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) waapishwa rasmi  
Habari MchanganyikoSiasa

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) waapishwa rasmi  

Spread the love

WABUNGE wa Bunge la Tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) jana tarehe 18 Disemba, 2022 wameapa rasmi kuanza shughuli za Bunge hilo Jijini Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katibu wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Alex Obatre ameongoza zoezi la kuwaapisha wabunge wapya kutoka Nchi Wanachama saba ambazo ni Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini, na Kongo DRC.

Wabunge wapya wa Bunge la Tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kutoka Tanzania waliopa ni Angela Charles Kizigha, Nadra Juma Mohammed, Dk. Shogo Richard Mlozi, Dk. Abdullah Makame, Machano Ali Machano, Mashaka Khalfan Ngole, Ansar Abubakar Kachwamba, James Kinyasi Millya pamoja na Dk. Ngwaru Jumanne Maghembe.

Baada ya zoezi la kuapishwa kwa wabunge hao, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax ambaye pia ameapishwa kama Mjumbe wa Baraza la Maamuzi la Bunge la Afrika Mashariki (EALA) amesema kuwa matarajio ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa inaendeleza Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika sekta za biashara na uchumi.

“Kama nchi lengo letu kuu ni kukuza na kuendeleza biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni imani yetu kuwa wabunge hawa wapya watasimamia jambo hili ili kuweza kuingia kwenye soko kubwa zaidi na kuhakikisha kuwa Tanzania inajiimarisha zaidi kibiashara ndani ya Jumuiya,” alisema Dk. Tax.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameapishwa kuwa Mjumbe wa Maamuzi wa Bunge la (EALA).

Septemba 22, 2022 wabunge tisa wanaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la (EALA) walipatikana kufuatia uchaguzi uliofanywa na Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya wagombea kujieleza mbele ya wabunge hao Jijini Dodoma.

Aidha, shughuli itakayofuata siku ya Jumanne tarehe 20 Desemba 2022 ni uchaguzi wa Spika wa Bunge hilo pamoja na uchaguzi wa Tume ya Bunge hilo unaotarajiwa kufanyika tarehe 21 Desemba 2022.

1 Comment

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. … MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!