Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB wazindua akaunti ya kidijitali inayofunguliwa kwa buku tu!
Habari Mchanganyiko

NMB wazindua akaunti ya kidijitali inayofunguliwa kwa buku tu!

Spread the love

ZAMA mpya ya huduma za kibenki imejiri nchini baada ya Benki ya NMB kuzindua suluhisho la kisasa ‘NMB Pesa Akaunti’ ambayo ni akaunti Ya kidijitali inayomwezesha mteja kufungua na kuanza kuitumia ndani ya dakika mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo inatajwa kuwa itaongeza msukumo mpya katika jitihada za taifa za ujumuishwaji wa kifedha na upatikanaji wa huduma za fedha  kidijitali kwa njia rahisi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akimsikiliza Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB, Filbert Mponzi wakati akimueleza juu ya mfumo wa malipo kwa kuskani QR (lipa Mkononi) ya Benki ya NMB katika moja ya Duka lililopo kwenye Stendi ya Mabasi ya Magufuli mara baada ya kuzindua NMB pesa Akaunti ya Benki ya NMB.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Magufuli jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi amesema sifa kubwa ya suluhisho la NMB Pesa Akaunti ni kuwa na mchakato mfupi wa kufungua akaunti mpya.

“Hili ni suluhisho litakalosaidia kutatua changamoto za kifedha ambazo mbali na akaunti kufunguliwa hapo hapo mteja alipo lakini pia utaweza kupata mikopo isiyo na dhamana, kutoa, kuweka au kutuma fedha, kulipia bili mbalimbali na kubwa zaidi haina gharama za ada za mwezi,” Mponzi alisema.

Aliongeza kuwa pindi usajili wa mteja mpya unapokamilika, akaunti yake itafunguliwa mara moja na kuanza kutumika moja kwa moja wakati huo ikiruhusu upatikanaji wa huduma zote za msingi kama ile ya NMB Mkononi.

Alisema ufunguaji huo mpya wa akaunti unafanyika mahala popote kwa Sh 1000 pekee na hauhusishi karatasi ya aina yoyote na mfunguaji haitaji kwenda wala kufika katika matawi 228 ya NMB yaliyotapakaa nchi nzima.

Mponzi alimweleza mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Amos Makala kuwa mwaka 2022 ulipoanza lengo la NMB lilikuwa ni kufungua akaunti mpya milioni moja.

“Mpaka sasa zimefunguliwa 1,012,344. Hii ndio maana halisi ya huduma za kifedha jumuishi Tanzania,” alisema.

Aidha, Makala alisema NMB Pesa Akaunti ni fursa kwa Watanzania wote kuwa na akaunti ya benki.

“Kwq sababu ufunguaji huo wa akaunti unafanyika kwa msaada wa wafanyakazi wa mauzo wa benki hiyo kwa njia ya simu za mkononi za aina zote.

“Kwa hiyo umahiri wa ubunifu wa NMB na uwekezaji wake katika teknolojia mpya umeijengea heshima kubwa nchini benki hii na kuifanya itambulike kimataifa,” alisemq.

Kwa mwaka huu pekee, NMB imekusanya zaidi ya tuzo 20 za kimataifa ilizotunukiwa na majarida yanayoheshimika duniani kama vile World Economic Magazine, Global Brands Magazine, International Banker Awards na International Business Magazine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!