Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi 13,000 Bunda wawalalamikia wateule Rais Samia
Habari Mchanganyiko

Wananchi 13,000 Bunda wawalalamikia wateule Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

WANANCHI zaidi ya 13,000 wa vijiji vinne vya Kata ya Nyatwali Wilaya ya Bunda mkoani Mara wameulalamikia uongozi wa wilaya hiyo kwa kile wanachodai kutumia jina la Rais Samia Suluhu Hassan kutaka kuwapora maeneo yao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakizungumza na MwanaHalisi Online baada ya kikao kati yao na uongozi wa wilaya kuvunjika, wananchi hao walisema Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) Salimu  Cherera anataka wananchi hao waondoke kwa madai kuwa amepokea waraka kutoka kwa Rais Samia ukiwataka wakazi hao waondoke mara moja.

“Katibu Tawala Cherera alikuja kama mlivyoshuhudia kwenyewe kikao amesema kuwa Rais ameandika waraka wa kutaka wakazi wa vijiji vinne vya Kata ya Nyatwali ambavyo ni Kariakoo, Tamau, Serengeti na Nyatwali kuondoka mara moja,” Alisema Diwani wa Kata ya Nyatwali Malongo Mashimo.

Aliendelea kusema “Sisi wananchi wa vijiji hivi tunaonewa na kutishiwa maisha na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Katibu Tawala na genge lake.

“Desemba 8,2022 Katibu Tawala huyo aliambatana na kundi la askari Polisi pamoja na  mwekezaji bila kuwepo diwani wa Kata ya Nyatwali na kuitisha kikao kibabe na akawa mwenyekiti wa kikao hicho”.

Diwani Malongo alisema Katibu Tawala huyo aliendesha kikao hicho na ajenda kuu ilikuwa ni kwamba Rais Samia ameagiza watu wote wa Kata ya Nyatwali kuondoka mara moja katika maeneo yao.

“Baada ya tamko hilo uongozi wa kata ulianza kuhoji kwa nini Katibu Tawala aendeshe kikao kwa niaba ya Diwani wakati si utaratibu, pia polisi wengi kiasi hiki kwani kuna vita?

Tuliomba kuonyeshwa waraka huo unaodaiwa umetoka kwa Rais Samia, lakini Katibu Tawala  alituambia kuwa sisi kwa vyeo vyetu haturuhusiwi kuonyeshwa nyaraka za Serikali,” alisema Malongo.

Diwani Malongo alisema Desemba 12,2022 kilifanyika kikao cha viongozi wa Kata alichokiandaa  yeye kwa agizo la Katibu Tawala ambapo DAS alifika na timu yake na baadhi ya maafisa aliodai wametoka Ikulu kwa madai kuwa wametumwa na Rais Samia hakuwatambulisha kwa majina na aliwaagiza viongozi wote wa Kata kuzima simu zao na kwamba akigundulika mmoja ajazima atachukuliwa hatua kali.

“Ajenda ya kikao ilisomwa na Katibu Tawala kuwa amekuja na timu yake kutufahamisha agizo la Rais Samia la kutuhamisha, viongozi tuliomba tuonyeshwe waraka huo, ambapo DAS alitoa waraka wa maelekezo ya nchi ya jumla ambayo yanataja namba ya (Stiki) ambapo sisi viongozi wa Kata tulianza kuhoji ni wapi kwenye waraka huo kata ya Nyatwali na vijiji vyake vinne imeajwa? Kikao kikavunjia watu wakatawanyika” Alisema Diwani Malongo.

Nao wazee wa Kata hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bunda Alfredi Malagira (80) Pamoja na Katen Mstaafu Richard Chacha wao wamesema watapigania haki ya wakazi wa Nyatwali mpaka mwisho kwani jambo hilo lilianza tangu mwaka 2002 lakini dhuruma hiyo ilidhibitiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mei 12,2014 kwa barua No PM/P/1/569/15.

Waliendelea kusema kuwa kana kwamba hiyo haitoshi Rais John Pombe Magufuli alizuia dhuruma hiyo kwa barua iliyoandikwa  Januari 15,2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu wakati huo Gerson Msigwa.

Naye Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Alfredi Malagira  alisema wanashangaa uongozi wa Wilaya kuja na suala hili kwa kutumia nguvu kubwa ya polisi na maneno ya kumsingizia Rais Samia kuwa kaagiza wananci  kuondolewa katika eneo hilo.

“Kutokana na hali hiyo tumefunga safari kutoka Bunda kuja Dar es Salaam kumuona  Makamu Mwenyekiti wa CCM Abrulhaman Kinana ili atupeleke kwa Rais Samia kufikisha kilio chetu hiki”.Alisema Malagira.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda  Salimu  Cherera alisema kuwa “Sisi tunaendesha vikao na wananchi wa eneo husika hatuzungumzi na watu wengine watafute wao watakueleza kinachoendelea.

“Sisi tunaheshimu sana vyombo vya habari kama unataka kujua suala hili funga safari kuja Bunda tutakupa ufafanuzi kwanini tunataka kuwahamisha”. Alisema Cherera.

Juhudi za kumpata Mkuu wa Wilaya ya Bunda Joshua Nasari zimegonga mwamba kwa takriban wiki mbili sasa kutokana na simu yake kutokupokelewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!