March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NEC yavikumbusha vyama kanuni za kampeni

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wake, Ramadhan Kailima

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewaomba wagombea watumie kanuni walizofundishwa katika kampeni za udiwani zinazoendelea katika kata mbalimbali nchini, anaandika Angel Willium.

Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima amesema wameruhusu mikutano ya kampeni katika uchaguzi wa madiwani, kwa lengo la kuhamasisha wanachama wa eneo husika wajitokeze kupiga kura.

Kailima amesema katika kampeni hizo mgombea mwenyewe au mtu anayeona anafaa anaruhusiwa kufanya kampeni lakini litakapotokea uvunjaji wowote wa maadili kama vurugu, mwanachama kuchana bendere ya chama kisichomuhusu, malalamiko watapeleka kwenye ngazi ya kata husika.

“Kwa mujibu wa kanuni kampeni zitaanza saa moja asubuhi hadi saa 12 jioni, kama kutatokea ukosefu wa amani waende kutoa malalamiko kwenye ngazi ya kata, na hatua zitachukuliwa,” amesema Kailima.

Kailima amesema mpaka sasa vyama vinavyoshiriki uchaguzi wa madiwani ni 12 na wagombea wawili wa vyama tofauti wamejitoa , hivyo wagombea wapo 152.

Aidha Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema siku ya uchaguzi wananchi watakiwa kwenda kupiga kura na siyo siasa, orodha ya wapiga kura itabandikwa Novemba 19, 2017 hivyo wanatakiwa kwenda kuhakiki majina.

Jaji Kaijage amesema daftari la kudumu la wapiga kura litakalotumika katika uchaguzi huo mdogo ni lile la wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, watakao piga kura ni wale waliojiandikisha kwenye uchaguzi mkuu.

Uchaguzi mdogo wa Madiwani, unatarajia kufanyika Novemba 29, 2017 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 12 jioni na mpiga kura aliyepoteza kadi ya kupigia kura au kadi imeharibika hawezi kuruhusiwa kutumia vitambulisho vilivyoruhusiwa na Tume.

error: Content is protected !!