Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea ataka wanasiasa waliofilisi TTCL wakamatwe
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea ataka wanasiasa waliofilisi TTCL wakamatwe

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo (Chadema)
Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea, ameitaka serikali kuwakamata na kuwafikisha mahakamani, watumishi wa umma na wanasiasa waliochangia kufilisika kwa shirika la simu la taifa (TTCL) anaandika Dany Tibason.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma leo Jumanne, Kubenea alisema, kampuni ya simu ya TTCL ilifilisika kutokana na kuhujumiwa na baadhi ya watu wenye mamlaka serikalini.

Kubenea amesema, kwa mujibu wa rekodi na taarifa zilizopo serikalini, muwekezaji aliyopewa TTCL wakati huo, alishindwa kutimiza masharti ya mkataba, lakini serikali iliendelea kumbeba na kumkumbatia.

Mbunge huyo machachari wa Chadema alikuwa alitoa kauli hiyo wakati aakijadili muswaada wa kuanzisha Shirika la Simu la umma (The Tanzania Telecommunications Bill, 2017).

Katika mchango wake huo, Kubenea alinukuu kauli ya aliyekuwa waziri wa Mawasiliano na uchukuzi, Prof. Mark Mwandosya aliyesema kuwa ubinafsishaji wa mashirka ya umma ilifanyika kutokana na serikali kushindwa kuyaendesha.

Kubenea alisema, Prof. Mwandosya alionya kuwa pamoja na dhamira njema ya kuanzisha mashirika ya umma, lakini kuyaendesha mashirika hayo na kuyasimamia, ni jambo lisilowezekana.

“Serikali iliamua kubinafsisha TTCL baada ya kujiridhisha kuwa teknolojia ilikuwa imebadilika na kuliendesha kunategemea ruzuku kutoka serikalini. Kulirudisha leo, ni kujipeleka mbele na kujirudisha nyuma,” ameeleza Kubenea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!