TUME ya Taifa ya Uchaguzi, imeteua wagombea 58 kugombea ubunge wa Mbarali mkoani Mbeya pamoja na udiwani katika kata mbalimbali nchini kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Septemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Agosti 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Emmanuel Kawishe wagombea hao wametoka katika vyama vya siasa 17 vilivyopata usajili kamili, ikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT-Wazalendo, ADA-TADEA, ADC, Chama cha Kijamii (CCK), Demokrasia Makini, TLP na NCCR Mageuzi.
NEC imeitisha uchaguzi mdogo baada ya Mbunge wa Mbarali, Francis Mtega, kufariki dunia tarehe 1 Julai 2023, kwa ajali ya kugongwa na treka.
Katika hatua nyingine, taarifa ya Kawishe imesema kata sitazitafanya uchaguzi mdogo, ikiwemo Kata ya Nala iliyopo mkoani Dodoma. Mfaranyaki (Ruvuma), Mtyangimbole (Ruvuma), Mwaniko (Mwanza), Old Moshi Magharibi (Kilimanjaro) na Marangu Kitowo (Kilimanjaro).
“Tarehe 5 Agosti 2023, tume ilitangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania bara na uteuzi wa wagombea umefanyika tarehe 19 Agosti 2023, kampeni za uchaguzi zimeanza tarehe 2Agosti 2023 na zinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 18 Septemba 2023,” imesema taarifa ya Kawishe.
NEC inateua wagombea? Du hii ya mwaka
Hawateuliwi na vyama vyao?