Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC: Uchaguzi Mbarali Septemba 19
Habari za Siasa

NEC: Uchaguzi Mbarali Septemba 19

Spread the love

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Mbarali na madiwani katika kata sita za Tanzania Bara, na uchaguzi utafanyika tarehe 19 Septemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima amesema NEC ilipokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Mbarali, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Francis Mtega.

Kailima amesema wagombea watachukua fomu kuanzia tarehe 13 hadi 19 Agosti 2023, siku ya uteuzi itakuwa tarehe 19 Agosti 2023 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 20 Agosti 2023 hadi tarehe 18 Septemba, 2023.

Amezitaja kata zitakazofanya uchaguzi mdogo kuwa ni Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mkoani Dodoma, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi na Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Pia kata ya Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

NBC yazindua kadi uanachama msalaba mwekundu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!