POLISI wa Jimbo la Massachusetts, limedai chanzo cha kifo cha Tafari Campbell (45), aliyekuwa mpishi wa Rais mstaafu wa Marekani,Baraka Obama, kilikuwa ni ajali na si mauaji kama ilivyodhaniwa. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo, kwa msaada wa mashirika ya kimataifa … (endelea).
Chanzo kimetajwa jana Alhamisi, baada ya Polisi kumaliza kufanya uchunguzi wake kuhusu kifo hicho, baada ya kuibuka madai kwamba marehemu Campbell aliuawa katika mazingira yenye utata.
Baada ya Polisi kutaja chanzo hicho, Mke wa Obama, Michelle Obama, kupitia ukurasa wake wa Facebook, aliandika ujumbe kuhusu Campbell, akieleza hisia zake za kumkosa baada ya kufariki dunia ,huku akituma salamu za pole kwa familia yake.
“Nitamkumbuka rafiki yangu Tafari, upweke wake utakuwa ni mgumu kwetu ila naahidi kubaki kuwa mwenye nguvu, kuendelea kuishi na kuheshimu urithi wake kwa kila njia. Pumzika kwa amani, kaka yangu,” ameandika Michelle.
Campbell alifariki dunia tarehe 23 Julai 2023, baada ya kutumbukia katika Bwawa lilioko karibu na nyumba ya Obama, iliyoko Kisiwa cha Martha’s Vineyard, kisha Mwili wake kupatikana tarehe 24 Julai mwaka huu, ukiwa ndani ya futi 100 kutoka katika usawa wa bwawa hilo.
Kabla ya kuwa mpishi wa Obama, Campbell alikuwa mpishi wa Ikulu ya Marekani, maarufu kama White House.
Leave a comment