Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo NBC yanogesha Derby ya Kariakoo kwa kampeni maalumu kujivunia mafanikio
Michezo

NBC yanogesha Derby ya Kariakoo kwa kampeni maalumu kujivunia mafanikio

Spread the love

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana Jumapili ilinogesha shangwe za mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kwa kuwapeleka uwanjani wateja wake pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo ili kushuhudia mtanange huo ulioisha kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Aidha, benki hiyo pia iliandaa matukio mbalimbali kwa ajili ya mashabiki wa soka pamoja na wateja wake katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam na Mwanza huku pia ikitumia mechi hiyo kubwa kuzindua rasmi kampeni maalum ya msimu wa huu wa soka inayofahamika kama ‘Soka Limeitika’ ambayo inalenga kuhamasisha na kujivunia mafanikio ya mchezo huo kutokana na udhamini wake kwenye ligi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wateja pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa na wadau hao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga iliyoisha kwa kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba.

Katika tukio hilo lililofanyika Dar es Salaam, ilishuhudiwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi akiongoza hafla fupi ya chakula cha mchana maalum kwa ajili ya baadhi ya wateja wakubwa na wadau wengine wa benki hiyo, tukio lililofuatiwa na msafara maalum kuelekeaUwanja wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo.

“Tumetumia mechi hii kubwa ili kwa pamoja tuweze kujumuika na kufurahia sambamba na wadau wetu hawa muhimu. Lengo ni kupata wasaa mzuri ili kufurahia pamoja ile ladha ya mchezo huu pendwa. Wote kwa pamoja tutakwenda uwanjani katika msafara maalum na baada ya mechi tutarudi pamoja kutoka uwanjani hadi hapa hotelini kisha tutaachana huku kila mmoja akienda kwake akiwa salama kabisa,’’ alibainisha Sabi.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wateja pamoja na wadau mbalimbali wa benki ya NBC waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa na wadau hao kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushuhudia mechi ya derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga iliyoisha kwa kwa timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 5 -1 dhidi ya Simba.

Akizungumzia kwa kina kuhusu kampeni ya ‘Soka Limeitika’  Meneja Masoko wa benki ya NBC, Alina Kimaryo alisema mbali na kuhamasisha ari ya mchezo huo pendwa, kampeni hiyo inalenga kujivunia mafanikio ya mchezo huo yaliyopatikana kutokana na udhamini wa benki ya NBC kwenye ligi hiyo inayozidi kujiongezea umaarufu barani Afrika na ulimwengu kwa ujumla.

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Brendansia Kileo akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wateja pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo.

“Tangu tuwekeze nguvu kwenye ligi hii benki ya NBC na wadau wa mchezo wa soka tumeshuhudia mafanikio mengi ya kujivunia ikiwemo kuongezeka kwa ubora wa ligi yetu kitaifa na kimataifa  ambapo nafasi ya ubora wa ligi yetu kwa viwango vya bara la Afrika kwasasa ni nafasi ya 5 kutoka nafasi 12 tuliyoikuta wakati tunaanza udhamini wetu.

“Pia udhamini wetu umeviongezea uwezo wa kiuchumi vilabu vinavyoshiriki ligi hii na sasa vipo imara kwenye eneo hilo na ndio sababu sasa hata mechi zinafanyika kulingana na ratiba bila vilabu kukwama kufika viwanjani kutokana na ukata,’’ alibainisha.

Aidha, alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na utoaji wa Bima za afya kwa wachezaji, familia zao na bechi la ufundi, mikopo ya mabasi inayolendelea kutolewa na benki hiyo kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi hiyo, ubora wa viwanja, udhamini wa benki hiyo kwenye ligi ya NBC Championship na ligi ya Vijana (Youth League) sambamba na uboreshaji wa huduma ya mauzo ya tiketi za michezo ya ligi hiyo kupitia mawakala wa benki hiyo waliopo maeneo mbalimbali nchini.

“Ni wazi kwamba udhamini wa NBC umeongeza vipato kwa vilabu ndio sababu sasa tunashuhudia vilabu vinaweza kusajili kwa ushindani wachezaji bora kutoka ndani na nje ya nchi hatua ambayo inaviwezesha kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.  Hamasa hii inayoshuhudiwa sasa kwenye mchezo huu pia ni matunda ya udhamini wa NBC na hiyo ndio maana halisi ya ‘Soka limeitika,” alimalizia Alina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

error: Content is protected !!