Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Biashara Jux afunika katika uzinduzi wa OPPO
Biashara

Jux afunika katika uzinduzi wa OPPO

Spread the love

 

MSANII wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Jux amekonga mioyo ya mashabiki wake Kwa burudani Kali wakati akitangazwa kuwa balozi wa Bidhaa za Kampuni ya Simu ya OPPO ambayo imezindiliwa rasmi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Msanii huyo aliwanyanyua wafanyakazi na wageni waalikwa ambao waliimba na kucheza nyimbo za msanii huyo katika uzinduzi wa OPPO.

Jux alisema ni fahari Kwa wasanii wa kitanzania kupata nafasi kama hizi za ubalozi wa bidhaa kwani ni njia moja ya kupata kipato na kujitangaza zaidi.

“Hii ni kampuni kutoka China lakini wameona umuhimu wa kuwekeza Tanzania Kwa sababu ya mazingira Bora yaliyowekwa na serikali lakini pia wameona umehimu ya kutumia kutangaza bidhaa zao,” alisema.

Wahamasishaji wengine ni Rommy Jones. Official 9 na DJ Mummy.

Mkurugenzi Mtendaji wa OPPO Tanzania, Kenny Yue alitangaza rasmi kuingizwa katika soko laTanzania bidhaa zake nchini Tanzania zijulikanazo ka ‘OPPO A series’.

Yue alisema kuwa kwa kawaida mtumiaji wa simu anaangalia vipengele muhimu wakati wa kubadilisha simu za mkononi, ikiwemo matatizo ya kiufundi, bei, huduma za kibunifu, chapa, umahiri na sifa nyingine nyingi za kimsingi, ndio maana OPPO imeshughulikia vipengele hivi vyote.

Alisema OPPO ilianzishwa mwaka wa 2008, na hadi sasa imejiweka vizuri kutoa teknolojia iliyo bora kwa watumiaji wake, na kuongeza kuwa kwa sasa kampuni hiyo inajivunia kuwahudumia watumiaji katika nchi zaidi ya 60 ulimwenguni.

“Tangu kuingia kwetu kwa mara ya kwanza katika bara hili la Afrika, OPPO imekuwa na mafanikio katika masoko mbalimbali katika nchi kama vile Misri, Morocco, Kenya na Afrika Kusini, na kuingia kwetu Tanzania ni uthibitisho wa dhamira yetu isiyoyumba ya kuifanya dunia kuwa mahali pa furaha kupitia teknolojia bora kwa watumiaji wetu wote, “alisema.

Alisema kuwa ripoti za hivi karibuni kutoka Canalys zimeonyesha hisa ya soko ya OPPO imekua kwa asilimia 73 kila mwaka, ikishika nafasi ya 4 katika bara la Afrika.

“Hii inaonyesha kuwa uwekezaji wetu katika masoko mapya kama vile Tanzania unaendelea kuonyesha imani na kujitolea kwetu kwa watumiaji wetu,” aliongeza.

Kuhusu bidhaa mpya katika soko la Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema mbali ya bidhaa zao za aina ya A Series, OPPO Tanzania inakusudia kutambulisha bidhaa zake za hadhi ya juu sokoni hivi karibuni, kama vile mfululizo wa Reno10 na Find N series.

“Tunapoanza safari hii ya kusisimua, tunawahakikishia wateja wetu kuleta teknolojia bora na bidhaa katika soko hili,” Farida Mwangosi, Meneja wa Bidhaa wa OPPO alisema.

Alisema kuwa OPPO inapeperusha bendera yao katika zaidi ya nchi 60, ikiwa na zaidi ya wafanyikazi 40,000 waliojitolea kuhakikisha wateja wao wanapata bidhaa na huduma bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Mwenge

Spread the love  KAMPUNI ya Meridianbet imefika maeneo ya Mwenge jijini Dar-es-salaam...

Biashara

Serengeti yakabidhi mkwanja kwa mshindi wa Maokoto ndani ya Kizibo

Spread the love Mshindi wa Maokoto ndani ya kizibo kutoka Kahama Mjini...

Biashara

Ushindi rahisi unpatikana kila ukicheza kasino ya Hot Joker

Spread the love  HOT Joker Fruits 20 ni mchezo wa sloti ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!