Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Nape awatahadharisha wanahabari kuhusu mikutano ya hadhara
Habari Mchanganyiko

Nape awatahadharisha wanahabari kuhusu mikutano ya hadhara

Spread the love

 

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye, amewataka waandishi wa habari kufuata maadili ya kitaaluma wakati wanaripoti mikutano ya hadhara, ili kuepusha habari ambazo zinaweza kuligawa Taifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Nape ametoa wito huo hivi karibuni akizungumza na wanahabari, ikiwa ni siku chache baada ya vyama vya siasa nchini kutangaza kusudio la kuanza kufanya mikutano ya hadhara, kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan, kuondoa zuio la mikutano hiyo lililowekwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli.

“Sio kila kitu ni stori, kwa sababu tunapeleka kwa mwingine kile tunachoandika, wito wangu uhuru uliotolewa wa mikutano ya hadhara utumike vizuri, turekodi yale ambayo yana faida kwa nchi yetu. Kama kukosoa tukosoe kwa ukweli, tukabalance stori na tukumbuke tuna wajibu wa kuhakikisha taifa hili linakuwa moja likiparanganyika wanahabari hamko juu ya hili,” alisema Nape.

Waziri huyo wa habari, aliwataka waandishi wa habari kutoandika maudhui yenye matusi, pamoja na kusikiliza pande zote mbili katika masuala yenye tuhuma ama madai (ku-balance stori).

“Tendeni haki kwenye stori zenu, msionee mtu m-balance stori zitakazotokana na mikutano sababu tukibeba hivi tunaweza kuwapelekea watu kusiko na situ ku-balance lakini hakuna sababu ya kuchapisha matusi kama mtu umeenda mahali ametukana huyo muache atukane ondoka zao au toa neno zuri alilotoa,” alisema Nape.

Aidha, Nape alimshukuru Rais Samia kwa kuimarisha uhuru wa habari “ameongeza uhuru kwenye tasnia ya habari nadhani kuliko wakati wowote katika historia, sikumbuki toka nimekuja hatujakamata na wala hatujamfinya mtu. Ukikosea tutakutafuta tukushauri. Tumewapa uhuru lengo lake mtusaidie kuwa macho kuhakikisha rasilimali za nchi yetu zinafaidisha wengi.”

Katika hatua nyingine, Nape alisema wizara yake inafanyia kazi agizo la Rais Samia la kuzifanyia marekebisho sera zinazosimamia tasnia ya habari.

“Sisi serikalini Rais ametuagiza tufanye mapitio ya sera ya habari, tunaipitia na ni ndoto zetu kwamba mbele ya safari tuunganishe utangazaji na uchapishaji, vyombo vya habari vya elektroniki na vya print ili tuwe na sera moja na ndiyo maana ya Rais kutengeneza wizara moja,” alisema Nape.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!