Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgodi waiangukia Serikali uvamizi wachimbaji wadogo
Habari Mchanganyiko

Mgodi waiangukia Serikali uvamizi wachimbaji wadogo

Spread the love

UONGOZI wa Mgodi wa CANUCK uliopo Wilaya ya Msalala  kata ya Mwakanta kijiji cha Magung’humwa mkoani Shinyanga umeiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuzuia uvamizi wa wachimbaji wadogo kwenye eneo lao la mgodi walilopatiwa leseni kihalali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kahama …(endelea).

Wito huo umetolewa jana tarehe 8 Januari, 2023 na Meneja Rasilimaliwatu na utawala wa mgodi wa CANUCK, David Deogratius wakati akizungumza na MwanaHalisi online kuhusu shughuli mbalimbali za mgodi huo.

Meneja Rasilimaliwatu na utawala wa mgodi wa CANUCK, David Deogratius

Amesema kuondoka kwa watu hao kutawezesha kampuni yao kuongeza uzalishaji kwa maana uwezo wa kampuni kuzalisha zaidi upo.

“Ukianga kushoto na kulia mwa mgodi wetu kuna leseni za watu wengine lakini mbele yetu ndio kuna wachimbaji wadogo ambao wametuvamia tunajikuta tupo katikati ambako tunashindwa kujitanua ukizingatia leseni yetu imefika hadi huko.

“Niombe Wizara ya Madini kutusadia kulisukuma jambo hili licha ya kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa kamishna mkazi wa mkoa wa kimadini Kahama na mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga lakini tunaamini tutafanikisha kwa wakati iwapo Wizara ikilibeba suala hili.

“Changamoto hii ikiisha tutaongeza uzalishaji na kurudisha kikubwa kwa jamii inayotuzunguka kupitia mfuko wa uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (CSR),” amesema Deogratius.

Amesema kuwa kampuni hiyo ilipata leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika kijiji hicho tarehe 30 Julai, 2020 na kuanza shughuli za uchimbaji wa madini.

Amefafanua kuwa Kampuni hiyo hadi sasa imetoa ajira ya kudumu kwa wafanyakazi 270.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!