Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yakanusha uvumi wa Wanyama kusafirishwa Loliondo
Habari Mchanganyiko

Serikali yakanusha uvumi wa Wanyama kusafirishwa Loliondo

Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali
Spread the love

 

SERIKALI imekanusha taarifa za uwepo wa ndege iliyoingia hifadhini na kusafirisha wanyama na rasilimali ambapo imedai kuwa taarifa zilizosambazwa mitandaoni “ni uzushi na zenye nia ovu.” Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Kuanzia jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilisambaa video ikionesha ndege ikitua katikati ya pori na wasambazaji kutoa maelezo kuwa ni ndege ya mwarabu kutoka Dubai imeingia katika hifadhi moja huko Arusha na kubeba wanyama pori na kuwasafirisha nje.

Serikali imekanusha madai hayo kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msingwa, ambaye amewataka watanzania kupuuza habari hizo na kwamba ndege zinazoingia hifadhini ni zile zinazopeleka watalii.

“Mimi niwaombe watanzania tupuuze huu uzushi, ni watu wameamua kufanya kwa maslahi yao hakuna ukweli wowote. Viwanja vyetu vya ndege maeneo yetu ya hifadhi hakuna eneo hata moja ambalo ndege zimekwenda kubeba Wanyama na kuwasafirisha kwenda nje ya nchi,” amesema Msigwa katika sauti aliyoishrikisha kwenye mtandao wake wa Istagram.

“Kwenye maeneo yetu ya viwanja vya ndege kwenye hifadhi zetu na maeneo ya utalii ni kweli zipo ndege zinakwenda zinapeleka wageni katika utarratibu amabo umekuwepo wakati wote, zinapeleka wageni hawa wageni wanakuja kwaajili ya kufanya utalii wapo watalii wanakuja na ndege na mizigo yao, wanafanya shughuli zao wakimaliza wanaondoka,” ameongeza Msingwa.

Amesema ndege inayotajwa alishaitolea ufafanuzi na kwamba ilitua katika uwanjwa wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ikashusha mizigo na kisha kurudi ikiwa tupu.

“Ndege kubwa kama ile haiwezi kutua kutua Poreleti au sehemu yoyote ndani ya hifadhi,” amesema Msingwa.

Amesema wakati huu nchi inafurahia kukua kwa sektanya utalii baada ya kutolewa kwa filamu ya Royal Tour ambayo imeongeza mapato kutokana na kuimarika kwa utalii.

Amewahakikishia watanzania kuwa rasilimali za Tanzania zipo salama na vyombo vya ulizni na usalama vipo macho kuangalia rasilimali na kwamba mamlaka zote zipo macho kuangalia huko.

Amesema kama kuna mtu mwenye ushahidi awasilishe Serikalini na hhatua zitachukuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!