Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nape ataka ‘kina Lissu’ wasibezwe
Habari za SiasaTangulizi

Nape ataka ‘kina Lissu’ wasibezwe

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki (kulia). Kushoto ni Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama.
Spread the love

NAPE Moses Nnauye, Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, ameitaka serikali kutopuuza hoja na ushauri unaotolewa na wabunge wa upinzani kwani ushauri wao ni muhimu katika kubainisha mapungufu ya utendaji wa serikali, anaandika Dany Tibason.

Nape pia alikuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali 2017/2018, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza umuhimu wa serikali kutopuuza maoni ya kila mbunge kwani yana umuhimu wake.

“Kelele zisiturudishe nyuma, lazima tusonge mbele kwa sababu vita hii ni takatifu, lakini tusipuuze katika kelele nyingi kunaweza kukawa na ushauri mzuri ndani yake.

“Tupuuze wapinzani nadhani, hii vita ni ya kwetu wote, nchi hii ikifaidika na jambo hili ni la kwetu wote bila kujali itikadi za vyama, sasa tusitoboane macho, tusitupiane vijembe visivyo na sababu. Ni wakati wa kuileta nchi yetu pamoja, tukapigane vita na tuishinde,” amesema Nape.

Nape amesema mshikamano wa kitaifa ni muhimu badala ya nyufa za mpasuko kwa misingi ya itikadi za vyama vya siasa ambavyo si muhimu kuliko maslahi ya Taifa.

“Wapinzani na CCM na wengine wote ni vizuri tukaungana kama vita yeyote ama safari yeyote inaweza kuwa na mashimo na mabonde na kunaweza kuwa gharama na vita hii tukubali kuzilipa faida yake ni kubwa,” amesema Nape.

Katika hatua nyingine Nape amesema Rais Magufuli si wa kwanza kuendesha vita ya kutetea rasilimali za Taifa na hivyo si vyema baadhi ya wana CCM kuwabeza marais waliopita kana kwamba wao hawakuwahi kufanya chochote cha kulinufaisha Taifa.

“Juhudi za kuzilinda rasilimali za nchi yetu hazijaanza awamu ya tano, bali zilianza tokea awamu ya kwanza. Mwalimu Julius Nyerere yapo mambo aliyafanya katika kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa. Vivyo hivyo kwa Marais wa awamu ya pili, ya tatu na ya nne,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!