Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtendaji atumbuliwa akituhumiwa kufanya mapenzi ofisini, kuhonga fedha za Serikali
Habari Mchanganyiko

Mtendaji atumbuliwa akituhumiwa kufanya mapenzi ofisini, kuhonga fedha za Serikali

Mtendaji wa Kijiji cha Mbigili wilayani Kilosa, Briton Mshani
Spread the love

 

MTENDAJI wa Kijiji cha Mbigili wilayani Kilosa, Briton Mshani, amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kufanya mapenzi ofisini, pamoja na kumhonga mpenzi wake kiasi cha Sh. 1 milioni, ambazo ni fedha zilizokuwa katika akaunti ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kilosa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa, amesema kwamba Mshani amefukuzwa kazi baada ya baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kumtuhumu kwa rushwa na kufanya mapenzi ofisini.

“Mtendaji wa kijiji aliyoiba fedha halafu akamhonga nyumba ndogo akageuza ofisi ya kijiji kuwa gesti, ametoa hela kwa kuhamisha akaunti ya Serikali kwenda kwenye akaunti binafsi ya mwanamke wake, huyu ameshafukuzwa kazi,” amesema Mwasa.

Katika hatua nyingine, Mwasa ameagiza mtendaji huyo wa kijiji achukuliwe hatua za kisheria huku akiagiza mtu mwingine atafutwe kwa ajili ya kujaza nafasi yake.

Mbali na tuhuma hizo, Mshani alituhumiwa kuchukua fedha za wanakijiji kiasi cha Sh. 500,000 kwa ajili ya kuwasaidia kutatua mgogoro wa ardhi, hata hivyo alikanusha madai hayo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!