Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yapiga marufuku uuzaji viwanja 20/20
Habari Mchanganyiko

Serikali yapiga marufuku uuzaji viwanja 20/20

Spread the love

 

SERIKALI imepiga marufuku uuzaji wa viwanja visivyopangwa maarufu kama 20/20, kwa kuwa unakwenda kinyume cha sheria na kuzuia wananchi husika kupata huduma za kijamii kwa kuwa hawapangi maeneo ya majengo ya umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Marufuku hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 3 Januari 2023 na Waziri wa Ardhi Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, akizungumza katika mkutano wa wadau wa sekta ya milki Tanzania.

Waziri huyo wa ardhi amesema ukubwa wa kiwanja chenye ujazo mdogo cha mita za mraba kinatakiwa kuwa na upana wa mita 16 na urefu wa mita 25.

“Mfano kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 400 kinapaswa kuwa katika uwiano wa upana wa mita 16 na urefu wa mita 25, yaani uwiano wa moja kwa moja yaani 20/20 haikubaliki kitaaluma na hakuna kiwanja kinachokubalika kwa namna hii,” amesema Dk. Mabula.

Angeline Mabula, Waziri wa Ardhi Maendeleo ya Makazi

Dk. Mabula ameagiza kampuni zilizowauzia wananchi viwanja vya namna hiyo na kuwasababisha kuingia kwenye migogoro ya ardhi kuwarejeshea fedha zao.

“Bodi ya usajili wa wathamini kufanya uchunguzi wa kampuni zote zinazofanya kazi kinyume cha sheria ili hatua kali ziweze kuchukuliwa haraka. Aidha, naagiza kampuni binafsi za upangaji na upimaji ardhi na kampuni nyingine yanayojihusisha na masuala ya ardhi (Real Estate Agency), na mtu yeyote anayejihusisha na uuzaji wa vipande vya ardhi kwa mtindo huu, wasitishe kazi hiyo haraka na kurudisha fedha kwa wananchi kwa maeneo ambayo wamekutana na kadhia mbalimbali,” amesema Dk. Mabula.

Katika hatua nyingine, Dk. Mabula amesema Serikali inaendelea kufanya maboresho ya sera na sheria za ardhi ili kuimarisha sekta ya milki inayokuwa kwa kasi nchini, akisema kwa sasa iko katika mchakato wa kuandaa Muswada wa Sheria ya Mawakala wa Milki (Real State Agency)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!