Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rungwe azungumzia ruksa mikutano ya hadhara “tumeondoka zama za kutishana”
Habari za Siasa

Rungwe azungumzia ruksa mikutano ya hadhara “tumeondoka zama za kutishana”

Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa Chama cha Umma
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, amesema zama alizoziita za kutishana zimeondoka na kwamba vyama vya siasa vitakuwa sawa mbele ya Serikali na vyombo vya dola. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rungwe ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuondoa zuio la mikutano ya hadhara, wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo tarehe 3 Januari 2023.

“Tumepata matangazo yake (Rais Samia), ni faraja sana tutakwenda kufanya mikutano ya hadhara bila vizuizi na wale mapolisi sio wa upande mmoja watakuja kutulinda wote hivyo ni jambo la kufurahisha tumeondoka zile zama za kutishana , hawa ni chama tawala hawa ni vyama vingine hawavijui,” amesema Rungwe.

Rungwe amesema “ nafikiri sasa ni jambo jema tunasubiri kuona upande wa utekelezaji itakuwaje, tutaelewa kama polisi wameelewa kivyake na sisi tumeelewa kivyetu. Sina la kusema zaidi ya kutoa pongezi kwa Rais sababu hii siku imechelewa sana tulikuwa tunaisubiri tuwe huru tufanye kazi ya kuijenga Tanzania nzima.”

Akizungumzia sakata la deni la taifa, Rungwe amesema Serikali kukopa si jambo baya, lakini inatakiwa fedha hizo ziguse maisha ya wananchi moja kwa moja.

“Kukopa sio jambo baya, tangu zamani mtu anakopa na alichokopa anafanyia kazi. Kama kukopa bila kuwa na lengo si jambo zuri, watu wanalalamika mikopo imekuwa mingi na wananchi hali zao mbaya za maisha kwa hiyo nafikiri wangekopa halafu wakaangalia wananchi,” amesema Rungwe.

Rais Samia ameondoa zuio la vyama vya siasa lililowekwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, na kuvitaka vyama vya siasa kuitumia fursa hiyo vyema kwa kufanya siasa za kistaarabu na zenye lengo la kuleta maendeleo kwa taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!