March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtatiro aitosa CUF, amuunga mkono Rais Magufuli

Spread the love

JULIUS Mtatiro, Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha CUF, amejivua uanachama wa chama hicho na kuonesha nia ya kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Mtatiro ametangaza uamuzi huo leo tarehe 11, Agosti, 2018 mbele ya wanahabari katika mkutano wake uliofanyika kwenye Ukumbi wa Protea jijini Dar es Salaam.

Mtatiro amesema ameamua kuchukua uamuzi huo na kuhamia CCM ili kupata fursa ya kuifanyia nchi maendeleo, akidai kwamba ndani ya CUF aliikosa fursa hiyo.

“Katika tafakari yangu ya kuhama, nilipitia maeneo kama matano ambayo nimefanyia kazi, niliangalia ushiriki na mchango wangu kwenye siasa za CUF, mgogoro unaoendelea kukikumba CUF, eneo la tatu ambalo nimelitafakari kwa upana sana ushiriki wangu kama kijana na kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi, jambo la nne ajenda ya maendeleo ya nchi, la mwisho ni ustakabali wangu kuhusu masuala ya siasa,” amesema Mtatiro.

error: Content is protected !!