Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Nape Nnauye atoa neno kuhama kwa Mtatiro
Habari za Siasa

Nape Nnauye atoa neno kuhama kwa Mtatiro

Spread the love

NAPE Nnauye, Mbunge wa Jimbo la Mtama ametoa neno baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF Taifa, Julius Mtatiro kukihama chama hicho, akisema kuwa hamahama hiyo itumike kama fursa ya kujenga upya demokrasia. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Nape ametoa maneno hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo amesema hamahama hiyo pia itumike kama fursa ya kujenga uimara wa CCM.

Hata hivyo, Nape amesema uimara wa CCM unategemea ubora wa upinzani huku akifananisha na ushindani wa timu za Simba na Yanga.

“Kama msomi wa Sayansi ya siasa, naona hii ni fursa muhimu ya kujengwa kwa aina mpya ya vyama na siasa za upinzani nchini! Kwa demokrasia hamahama hii, ni muhimu itumike kama fursa ya kujenga upya uimara wa CCM unategemea ubora wa upinzani. (Simba/Yanga),” ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!