Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mtakwimu mkuu: Hii ndio tofauti ya sensa ya 2022 na zilizopita
Habari za SiasaTangulizi

Mtakwimu mkuu: Hii ndio tofauti ya sensa ya 2022 na zilizopita

Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Dk. Albina Chuwa
Spread the love

MKURUGEZI Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Dk. Albina Chuwa amesema sense ya watu na makazi itakayofanyika Agosti mwaka 2022, ni ya tofauti na sensa tano zilizopita kwani itakuwa ya kidijitali. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Dk. Chuwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 14 Septemba 20211 katika uzinduzi wa kitabu cha mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Amesema mkakati huo wenye sura tisa, umeeleza uzoefu uliopatikana sensa tano zilizopita, changamoo zilizopatikana.

“Umetueleza changamoto hizo kuwa ni fursa kwa sensa tunayokwenda kufanya. Sura ya tisa inazungumzia tathmini ya sensa ya mwaka 2022, kwamba viashiria gani vinakwenda kutumika katika kufanya sensa yetu,” amesema.

Amesema hadi sasa Tanzania imefanya sensa tano, lakini sensa ya sita inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022, ni sensa ya kipekee katika historia ya nchi tangu ilipopata uhuru mwaka 1961.

“Tofauti ya kwanza, sensa tano zilizopita tulitumia teknolojia ya makaratasi kwa asilimia 95, sensa ya nne ya mwaka 2012 tulitumia teknolojia ya scaning sensa ya nne ilitupa matokeo ndani ya miezi mitatu. Sensa ya mwaka kesho Agosti itatupa matokeo ndani ya mwezi mmoja.

“Sensa tano zilizopita tulikuwa tunatumia madodoso ya aina mbili, moja lenye maswali 64 kwa sensa ya mwaka 2012 na lingine fupi lilikuwa na maswali 20,” amesema.

Amesema katika uchambuzi wa sensa zilizopita, uchambuzi uliishia katika ngazi ya wilaya, watakwimu hawakuweza kwenda ngazi ya kata, kijiji na kitongoji.

“Ngazi ya kata, kijiji na kitongoji tulikuwa tunatoa idadi ya watu peke yake kwa sababu tulikuwa tunatumia teknolojia ya sampuli, asilimia 30, 40 kwa sense zilizopita.

“Tofauti kubwa sana na sensa zilizopita, Serikali inaenda kufanya mazoezi matatu makubwa ya kitaifa, tunaenda kuhesabu watu kwa kuchukua taarifa zao za kiumri, kijinsi, uraia, elimu na shughuli zote wanazofanya sambamba na makazi yao, hilo ni zoezi tosha tunaita traditional census kama ilivyoainishwa kwenye mapendekezo ya Umoja wa Mataifa.

“Katika sensa ya mwaka 2022 tunaenda kuongeza taarifa za majengo yote nchi nzima, vijijini na mijini. Tutaenda kukusanya aina ya paa, kuta, shughuli ndani ya majengo hayo… kama ni ghorofa sita makarani watapita jengo hadi jengo kupata wamiliki wote kwa nchi nzima. Hilo ni zoezi tosha,” amesema.

Rais Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe ikiwa ishara ya kuzindua Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022

Amesema zoezi lingine kubwa ni kuchukua anuani za makazi katika majengo yote ya nchi nzima kwa maeneo ya mijini na vijijini.

“Tunaenda kuchukua anuani ya kila jengo, barabara au mitaa inayozunguka majengo. Lengo ni kufahamika ipasavyo makazi yako wapi na tunaenda kuchukua taarifa zote na kuweka kwenye kanzi data ya taifa, ukibonyeza taap! pale Kariakoo unajua kuna duka la nani na lipo sehemu na unaweza kufuatilia.

“Hii ni fursa hususani kwa akina mama, tukiwa na anuani hizi ni rahisi sana kuweza kupata mikopo kwa akina mama, vijana na watu wote. Tukifanya hivi Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kwa Bara la Afrika,” amesema.

Aidha, ameongeza kuwa katika sensa hiyo, mipaka ya vitongoji vyote nchini itahuishwa rasmi na kuingizwa kwenye kanzidata ya Taifa pamoja na Shehia kwa upande wa Zanzibar..

“Kutakuwa na taarifa za kitakwimu ngazi ya kitongoji na mitaa zinazohusu hali ya uchumi wa jamii katika kitongoji, mazingira yao. Ni tofauti kubwa ambayo tunakwenda kuifanya,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!