July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aweso atua Bukoba, aagiza milioni 420 za mkandarasi zilipwe

Juma Aweso, Waziri wa Maji

Spread the love

 

WAZIRI wa Maji nchini, Jumaa Aweso amejionea hali ya mradi wa maji wa Kemondo-Maruku wilayani Bukoba Mkoa wa Kagera huku akitoa maagizo kwa mfuko wa taifa wa maji kupeleka Sh.420 milioni anazodai mkandarasi. Anaripoti Danson Kaijage, Bukoba … (endelea).

Aweso amesema hayo leo Jumanne, tarehe 14 Septemba 2021, katika ziara ambapo ametembelea ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa ujazo wa lita milioni tatu ambao kwa sasa utelezaji wake umefikia asilimia 35.

Katika Mradi huo, unatarajia kuhudumia wananchi wapatao 117,561 katika kata 6 zenye jumla ya vijiji 17.

Aweso ameuagiza uongozi mkuu wa mfuko wa taifa wa maji kuhakikisha unapeleka kiasi cha Sh. 420 milioni anazodai mkandarasi ili akamilishe ujenzi wa tanki hilo kwa wakati.

Katika hatua nyingine, viongozi wa Wilaya ya Bukoba na mkoa wa Kagera wameipongeza Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua ya kuwapelekea mradi wa kimkakati wenye thamani ya Sh.15.8 bilioni ambao utasaidia kupunguza adha ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa vijiji hivyo..

error: Content is protected !!