September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dakika 3 za Ali Kiba mbele ya Rais Samia

Ali Kiba

Spread the love

 

ALI Kiba, msanii wa muziki nchini Tanzania, ametumia takribani dakika tatu kutumbuiza mbele ya mamia ya wananchi wakiongozwa na Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Matlida Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa burudani hiyo asubuhi ya leo Jumanne, tarehe 14 Septemba 2021, katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma katika shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, inayofanywa na Rais Samia.

Ali Kiba aliitwa jukwaani saa 4:45 asubuhi kutumbuiza na kuwaburudisha kwa wimbo wake mmoja wa Ndombolo huku akishangiliwa na mamia waliojitokeza uwanjani hapo. Saa 4:48 akashuka jukwaani.

Amepanda jukwaani akiwa ameshika bendera ya Tanzania huku akiwa amevalia mavazi meusi yaani shati na jeans.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!