Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Zoezi la sensa sio geni, viongozi wa dini tusaidinieni
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Zoezi la sensa sio geni, viongozi wa dini tusaidinieni

Rais Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe ikiwa ishara ya kuzindua Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kwa kuwa zoezi la sensa sio geni… muda utakapofika kila Mtanzania ajitokeze kuhesabiwa kwani sensa ina faida nyingi. Anaripoti Glory Massamu TUDARCo … (endelea).

Amesema sensa inaisaidia serikali kufanya uamuzi sahihi kuhusu ugawaji wa rasilimali na kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 14 Septemba 2021 jijini Dodoma wakati akizindua kitabu cha mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Pia amewaomba viongozi wa dini pindi wanapokuwa katika mahubiri yao wasisahau kuhamasisha wananchi wajitokeze katika zoezi hilo litakapofanyika Agosti mwaka kesho.

“Sensa ya kwanza ilifanyika rasmi mwaka 1910, ya kisayansi ilifanyika 1967. Tangu wakati huo nchi imekuwa ikifanya sensa kwa wastani wa miaka 10 na mara ya mwisho ilifanya mwaka 2012.

“Zoezi hili ni kufahamu idadi ya watu, jinsia yao, elimu yao, hali zao, ajira zao, ubora wa makazi mahali yalipo na hali yake. Taarifa zitatusaidia idadi ya ongezeko la watu na hali ya uhamiaji.
Zitaiwezesha nchi kutambua taarifa za kupima maendeleo,” amesema.

Ameongeza kuwa sensa hiyo itaiwezesha serikali kuandaa sera ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu.

Amesema kwa kuwa taarifa za sensa zinatumiwa na jumuiya za kimataifa kufanya maamuzi mbalimbali ya kimaendeleo, ni vema taarifa hizo kutolewa na NBS badala ya asasi za kimataifa.

“Ili kukidhi mahitaji zoezi lazima lishirikishe watu wote, litahusisha watu wote watakokuwa wamelala ndani ya mipaka ya Tanzania kwani hii ndio tabia ya zoezi hili hivyo kuna umuhimu mkubwa kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hili,” amesema.

Aidha, amesema kupitia madodoso hayo ya sensa, watakwimu wanakwenda kupiga ndege wawili kwa jiwe moja yaani kuhesabu watu na makazi yao jambo ambalo halikuwahi kufanyika katika sensa zilizopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!