NAIBU waziri, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewataka watumishi wa umma, kutokimbia kufanya kazi pembezoni mwa nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Chalinze, leo Jumapili, Ridhiwani alisema, “hakuna sababu ya watumishi kuchagua mahali pakufanyia kazi.”
Aliwataka watumishi wa umma, kuendelea kuwahudumia wananchi wote sawa na hakuna sababu ya kuchagua na kuweka madaraja katika utoaji wa huduma.
Alisema, “…kutochagua vituo vya kazi, kunalenga sio tu kuwasaidia baadhi, lakini kunatengeneza madaraja katika utumishi wa umma.”
Akatumia mkutano huo kuwakumbusha watumishi umuhimu wa kufanya kazi kuzingatia misingi ya kazi ikiwemo kujitambua na kutambua tunaowahudumia.
Akaongeza: “Popote utakapopelekwa kuna hadhi ya mtumishi kuweza kufanya kazi. Nawaomba wazazi kuacha kupiga simu kuwaombea watoto wenu vibali vya kuhamishwa vituo ili wapelekwe mijini.”
Katika kikao hicho, Ridhiwani aliwapongeza watumishi wa halmashauri hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Leave a comment