Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mrema akubali muswada wa vyama vya siasa, aomba ruzuku
Habari za Siasa

Mrema akubali muswada wa vyama vya siasa, aomba ruzuku

Spread the love

MKONGWE wa Siasa Nchini na Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema, ameitaka serikali inapofanya marekebisho ya vyama vya siasa iweze kuangalia umuhimu wa kuvipatia vyama vidogo vya siasa ruzuku ili navyo viweze kujiendesha. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kutaka marekebisho hayo kuruhusu vyama vya siasa ambavyo havina wabunge wala madiwani kupewa ruzuku pia ametaka sheria iruhusu kufanyika kwa mikutano ya siasa ili kuweza kujenga vyama hivyo.

Mrema akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa yapo mambo ambayo katika marekebisho ya siasa lazima yaingizwe na kutoa nafasi sawa kwa vyama vya siasa vidogo na vikubwa kwani vyote vinafanya siasa za kulijenga taifa kwa misingi ya utaifa.

Katika hatua nyingine Mrema alivitaka vyama vya siasa vya upinzani kuangalia uwezekana kwa kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuusoma vyema muswada wa vyama vya siasa na kuona ni wapi kuna mapungufu ili yaweze kurekebishwa na yale mazuri yakubaliwe.

Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya Magereza alisema kuwa licha ya kuwa yeye ni mtumishi wa serikali kwa sasa lakini hawezi kufumbia macho mambo maovu ambayo yanafanywa na serikali na kama yatakuwepo atayasema.

“Mimi pamoja na kuwa mtumishi wa serikali lakini ikumbukwe kuwa nimeitumikia sana nchi hii kwa nafasi mbalimbali hivyo basi siwezi kunyamaza pale ninapoona mambo yanaenda vibaya lakini pia ninapoona mambo yanaenda vizuri nitasema ukweli,” alisema Mrema.

Hata hivyo Mrema alipoulizwa kama kweli yeye ni kibaraka wa wa Serikali kwa lengo la kutaka kuumiza vyama vingine na kutaka astaafu siasa ili aendelee na shughuli nyingine, alisema kuwa yeye ni mwanasiasa ambaye anapenda siasa na siyo kibaraka ila anapenda kusimamia ukweli.

“Siyo kweli kuwa mimi ni kibaraka wa serikali ya CCM ila mimi nataka kufanya siasa ambayo inaweza kuwa na tija haiwezekani nikaona serikali inafanya vibaya nikanyamaza lazima nitasema tu na kuikosoa serikali kwani mambo mangapi nimekuwa nikiyasema.

“Kwa mfano nataka serikali iruhusu mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote vya siasa kwani vyama vyote vinajenga nchi, lakini pia ikumbukwe kuwa vyama vyote vinatakiwa kupewa ruzuku ili viweze kujiendesha ili navyo viweze kupimwa kwa uhaminifu wa mapati,” alisema Mrema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!