Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wafikia asilimia 95.8
Habari Mchanganyiko

Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wafikia asilimia 95.8

Bwawa la Umeme Rufiji
Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameeleza kuwa Serikali imeamua kuwekeza katika miradi ya nishati ili kuhakikisha upatikanaji umeme unakuwa mkubwa kuliko mahitaji ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema hayo tarehe 18 Januari 2024 jijini Dodoma wakati wizara ya nishati ilipowasilisha taarifa kuhusu hali ya uzalishaji na usambazaji umeme nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Kikao ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, Katibu Mkuu, Mhandisi, Felchesmi Mramba, baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watendaji wa Wizara ya Nishati.

“Moja ya vipaumbele vikubwa vya Serikali ni sekta hii ya nishati na ndio maana fedha zimekuwa zikitolewa za kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati ikiwemo mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao gharama yake ni Sh 6.5 trilioni na mpaka sasa Serikali imeshamlipa mkandarasi Sh 5. 7 trilioni ambayo ni sawa na asilimia 88.7,” amesema Dk. Biteko

Kuhusu usimamizi wa mradi wa JNHPP amesema Serikali iko makini katika usimamizi  wake na kwamba kuna mamlaka mbalimbali zinazosimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa ufanisi akitoa mfano timu maalum ya wataalam iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kusimamia mradi huo ambayo inaongozwa na Profesa Idris Kikula.

Kuhusu hali ya miundombinu ya umeme nchini, Dk. Biteko amesema itaendelea kufanyiwa matengenezo ili iweze kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme kwa ukamilifu wake, huku juhudi za kujenga miundombinu mingine mipya ikiendelea.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alieleza kamati kuwa, mradi  wa umeme wa JNHPP kwa sasa umefikia asilimia 95.8 na kwamba mtambo namba tisa utakaozalisha megawati 235 umeshakamilika na mtambo namba nane na namba saba iko mbioni kukamilika.

Kuhusu hali ya umeme nchini, Mhandisi Nyamo-Hanga amesema kuwa, pamoja na jitihada mbalimbali zinazoedelea kufanywa na Serikali ili kupunguza changamoto ya umeme nchini, hali ya upungufu wa umeme itaisha mara baada ya kuwashwa kwa kwa mashine mbili za JNHPP zenye uwezo wa megawati 470 ambazo zinatarajiwa kuwashwa kabla ya mwezi Machi, 2024.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dk. David Mathayo David pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza viongozi wa wizara ya nishati kwa usimamizi mzuri wa sekta na kueleza kuwa wana imani kwamba viongozi hao kwa kushirikiana na taasisi zake wataiwezasha nchi kuwa na nishati ya kutosha, ya uhakika na inayotabirika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

error: Content is protected !!