September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Uhuru afunga mpaka Tanzania, Somalia

Spread the love

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema, kuanzia leo Jumamosi tarehe 16 Mei, 2020 saa 6 usiku, mpaka wa Kenya na Tanzania (Namanga) na wa Kenya na Somalia itafungwa kwa siku 30. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Amesema, mipaka hiyo hiyo itafungwa kwa abiria pekee, lakini magari ya mizigo ambayo nayo, madereva wake watapaswa kupimwa kuona kama hawana maambukizo ya virusi vya ugonjwa wa corona (COVI-19) ndipo watakaporuhusiwa kuingia na kutoka.

Akirihutubia taifa, Rais Kenyatta amesema, hatua hiyo inalenga kupunguza maambukizo ya corona ambayo yanaendelea kusumbua mataifa mbalimbali dunia.

“Wiki iliyopita, tumeshuhudia ongezeko la visa vya Covid-19 kutoka nje, ikiwemo watu wanaoingia nchini kupitia mipakani. Kesi 43 zinatokana na watu waliovuka mipaka ya Tanzania na Somalia,” amesema Rais Kenyatta.

Amesema kwa sasa Kenya ina wagonjwa 830 baada ya ongezeko la wagonjwa wapya 49.

Rais Kenyatta amesema wagonjwa 16 wameripotiwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya (Namanga)  wakati katika mipata ya Kenya na Somalia wamepatokana katika maeneo ya Wajir 14, Lungalunga (2), Loitoktok (1) na Isebania 10.

Rais Kenyatta ametangaza siku 21 zaidi za watu kutoka ndani katika miji ya Nairobi, Mombasa, Kwale, Kilifi na Mandela hadi tarehe 6 Juni, 2020 kuanzia saa 1 usiku hadi 11 asubuhi.

Wanaoishi katika maeneo hayo, hawaruhusiwi kutoka eneo moja kwenda jingine.

Amesema ugonjwa huo ni hatari na unasumbua nchi mbalimbali duniani ikiwamo Kenya hivyo, kuwaomba Wakenya  kushirikiana ili kuhakikisha ugonjwa huo unamalizika.

“Jukumu la kwanza la Serikali ni kuhakikisha tumelinda maisha na mali za watu. Kwangu mimi, ningekuwa nimewaangusha Wakenya kama nisipowaambia ukweli vile ulivyo,” amesema Rais Kenyatta.

Amewataka wananchi wa nchi hiyo kufuata taarifa za wataalamu na kuepuka kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine kama hakuna sababu ya msingi.

“Usichukue jukumu kwenda kuupeleka ugonjwa kwa wenzako, jamii, familia, baba, mama au mtu ambaye hana hatia yoyote ukampelekea ugonjwa,” amesema

Rais Kenyatta, ametolea mfano kijana mmoja aliyewatoroka askari kutoka Mombasa kwenda Machakosi ambapo baada ya kufika huko, akamwambukiza corona dada yake.

“Huu ugonjwa ni hatari, na yale masharti tuliyoyatoa lazima tuyatimize sisi Wakenya na siyo kwamba tunataka kuumiza watu hapana, tunataka kurudi makanisani, misikitini lakini mazingira hayaruhusu,” amesema.

error: Content is protected !!