MLINZI wa Hoteli ya Twiga, aliyefahamika kwa jina la Cyprian, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita, kwa tuhuma za kuchoma gari lililokuwa linatangaza mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).
Taariifa hiyo imetolew leo tarehe 2 Agosti 2023 na Kaimu Kamanda wa Polisi Geita, ACP Adam Maro, baada ya gari hilo lenye usajili T.658 DQL, kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo.
Kamanda Maro amesema uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea kufanywa na Polisi, huku akidai hadi sasa chanzo chake hakijajulikana.
Gari hilo lilikuwa linatangaza mkutano wa hadhara wa Lissu, unaotarajiwa kufanyika wilayani Chato, mkoani Geita, ambako ni nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli.
Lissu yuko katika ziara ya kikazi Chato, ambapo hivi karibuni alitangaza nia ya kwenda kuzuru kaburi la Hayati Magufuli, ambaye alikuwa anakosoa utawala wake alipokuwa madarakani kabla hajafariki dunia Machi 2021.
Jengeni hoja mumjibu baada ya hotuba yake. Wivu na chuki za kijinga na kitoto haziinuafaishi Afrika!