March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mkwara wa Lipumba wapagawisha wabunge wa CCM

Prof. Ibrahim Lipumba

Spread the love

HOFU ya wabunge kuvuliwa uanachama na kusababisha wapoteze nyadhifa zao za ubunge sasa imeanza kutanda ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Dany Tibason.

Wabunge wa CCM wakizungumza na Mwanahalisi Online, kwa masharti ya kutokutajwa majina yao wamesema kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba kuwavua ubunge wabunge wa viti maalum na Spika kuridhia hali hiyo kwa haraka ni dalili ambazo zinaweza kuhamia katika chama tawala.

“Sikiliza Broo hapa kuna mkakati mkubwa na wa maana wa kutaka kuwawajibisha wabunge ambao wanaweza kuonekana kuwa ni kihelehele na ujue bwana mkubwa ndiye mwenyekiti wa chama unadhana akitaka kukuondoa madarakani inashindikana,” amesema mmoja wa wabung.

Mbunge mwingine ambaye alizungumza amesema kuwa kwa sasa kuna changamoto kubwa ndani ya siasa na kikubwa zaidi ni kutojitokeza kutoa ushauri mbalimbali lakini tunatakiwa kufanya kazi.

Amesema Bunge linasubiri ripoti ambayo italetwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ya Bunge, huku akisema hakuna kipya katika ripoti hiyo.

Ameongeza kuwa kwa sasa Wabunge wa CCM , hawaaminiani kwa kuwa watumia jina la mwenyekiti wao.
Wiki iliyopita mbunge wa Nzega mjini (CCM), Husein Bashe aliomba mwongozo kwa Spika, akitaka maagizo kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kuvihoji vyombo vya ulinzi na usalama ili kupata majibu sahihi ya matukio yanayoendelea hapa nchini.

Bashe alilazimika kuomba mwongozo huo kutokana na kuvamiwa kwa Mwanasheria mkuu wa Chama cha Dempkrasiana na Maendeleo (Chadema), mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D akiwa anatokea bungeni.

Mbali na hilo Bashe amesema kuwa kumekuwepo na matukio mengi ambayo ni ya kutisha, lakini hakuna majibu sahihi yanayotolewa na vyombo vya dola huku mwisho wake matukio hayo yanaonekana kuwa ni ya kawaida.

error: Content is protected !!