March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mdee kumtusi Magufuli yapigwa kalenda

Halima Mdee (mwenye nguo nyeupe) akiwa mahakamani akisubiri kesi yake kutajwa kabla ya kuhairishwa

Spread the love

KESI inayomkabili mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), imepigwa kalenda hadi Oktoba 11,mwaka huu itakapoanza kusikilizwa, anaandika Hellen Sisya.

Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli.

Anadaiwa kutoa maneno hayo mwezi July mwaka huu, akiwa katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo katika mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Victoria Nongwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na anatetewa na mawakili watatu wakiongozwa na Wakili msomi Peter Kibatala huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na mawakili wawili wakiongozwa na wakili msomi, Mutalemwa Kishenyi.

error: Content is protected !!