Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkataba wa DP – Dk. Slaa aitisha mkutano wa hadhara, “Ubalozi chukueni”
Habari MchanganyikoTangulizi

Mkataba wa DP – Dk. Slaa aitisha mkutano wa hadhara, “Ubalozi chukueni”

Dk. Wilbroad Slaa
Spread the love

 

MWANASIASA mkongwe na Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Balozi Dk. Willbroad Slaa ametangaza kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22 mwezi huu kwa engo la kuelimisha wananchi kuhusu kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Mkataba huo uliosainiwa Oktoba mwaka jana na kuridhiwa na Bunge Juni mwaka huu ni kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia kampuni ya DP World. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo, tarehe 12 Julai 2023 jijini Dar es Salaam ameweka wazi kuwa hapingi uwekezaji katika bandari hiyo ya Dar es Salaam bali anapinga mkataba wa uwekezaji kwa kueleza kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

“Tutakwenda kwenye jimbo lenye watu wengi zaidi na uwezekano wa kwanza ni Viwanja vya Mbagala Zakheim, wa pili Tanganyika Peakers, au pale karibu na Airport.

“Nimetamka haya hadharani nikitambua kwamba kuna hila zinatumika ukipeleka ile barua Polisi unambiwa kuna chama kilishaomba mkutano… Polisi tuwe na mapenzi mema na nchi yetu tunachopigaia ni kwa ajili ya Watanzia sote” amesema Dk. Slaa.

Amesema uwekezaji huo hautaleta tija kwa nchi kwa sababu ya mkataba huo ni mbovu.

Aidha, Dk. Slaa ameeleza kuwa ametishwa licha ya kutoeleza kuwa ametishiwa kuvuliwa ubalozi wake.

“Najua maneno hayo ni makali… nimepokea vitisho na mimi pia sio tu Mawakili, wengine wakasema ubalozi wako tutachukua, nawaambia chukueni sasa hivi, siishi kwa ajili ya ubalozi. Nimesema sina chama najiamini najau ninachosimamia

“Nitasema siku zote, CCM au Chadema ikifanya mema nitapongeza, anayeharibu yeyote nitamsema bila kumung’unya maneno, bila kuona aibu na kwa hili hakuna aibu tutakwenda wote,” amesema.

“Hapa tatizo sio elimu tatizo mkataba ni mbovu kama mkataba ni mbovu hatuhitaji elimu kuhusu chochote… tukae meza moja tujadilianeni na wataaalamu tutafute njia ya pamoja kutoka katika msiba huu,” amesema na kuongeza kuwa;

“Msiba ukishaingia kwenye taifa au kijiji hukaa chini kutafuta wazee wenye busara kujadiliana namna gani watoke kwenye msiba huo,” amesema.

Dk. Slaa ameeleza kuwa amepata uzoefu akiwa amehuduma kama mbunge wa Karatu kwa muda wa miaka 15 kuanzia mwaka 1995 mpaka 2005.

“Nina uzoefu wa kukaa bungeni miaka 15 nimeona mikataba ya serikali kipindi hicho, najua mema yote yaliyofanyika katika uwekezaji nzuri ninajua mabaya katika uwekezaji mbaya kwa hiyo ninapozungumza nazungumza nikiwa na ushahidi wa kina,”amesema.

Aidha, Dk Slaa aliungwa mkono na Mkuu wa Kanisa na Moravian la Uamsho la Tanzania na Afrika Mashariki, Askofu Emmaus Mwamakula ambaye alikuwa ameambatana naye kwamba kila Mtanzania anao uhuru wa kutoa maoni kuhusu mkataba huo bila kubughudhiwa.

Aidha, ameeleza kushangazwa na kitendo cha Polisi kumhoji Wakili wa kujitegemea Dk. Rugemeleza Nshala kwa kutoa maoni ilhali ilitakiwa wafuatilie malalamiko yake ya kutishiwa kuawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

error: Content is protected !!