Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mjane wa Mrema aonja urithi, utata wa ndoa wamalizwa
Habari za SiasaTangulizi

Mjane wa Mrema aonja urithi, utata wa ndoa wamalizwa

Spread the love

Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke kimetoa uamuzi juu ya urithi wa mali za marehemu Augustino Lyatonga Mrema ambapo imemtaja mjane wa Mremba Doris kuwa mnufaika wa mirathi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa tarehe 20 Oktoba na Jaji Augustine Rwizile  ambapo ameeleza kuwa Peter Mrema ndiye msimamizi pekee wa mali zilizoachwa na marehemu Mrema huku  mjane wake akikataliwa kuwa msimamizi wa mali hizo.

Katika uamuzi huo umewaorodhesha watu tisa watakaonufaika ambao ni pamoja na Doris Agness Augustin Mkandala (45) ambaye ndiye mjane wa Mrema, Elizabeth Augustino Mrema (52), Mary Augustino Mrema (48),  Cresencia  Augustino Mrema (45), Elizabeth  Augustino Mrema (43), Michael Augustino Mrema  (40), Edward Augustino Mrema (38), Peter Augustino Mrema (37), na Godlove Augustino Mrema (18).

UTATA WA NDOA WAMALIZWA

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mtoto wa Mrema, Peter Augustino Mrema kuwasilisha ombi katika mahakama hiyo la kutaka mjane wa marehemu, Doris aondolewe katika usimamizi wa mali na wala asihusishwe kwa kuwa hakuwa mke halali wa marehemu baba yao.

Pia Peter alitaka baadhi ya watoto wa marehemu wasihusishwe katika ugawaji wa mali hizo jambo ambalo mahakama pia imelipinga.

Hata hivyo, uamuzi huo umedai kuwa ndoa aliyofunga Mrema na Dorris tarehe 24 Machi 2022 katika Kanisa Katoliki Parokia Uomboni, Marangu mkoani Kilimanjaro, ni ndoa halali.

Mahakama hiyo imedai kuwa licha ya Doris kukiri kuwahi kufunga ndoa kabla ya kufunga ndoa ya pili na Mrema, tayari ndoa yake ya kwanza ilikuwa imeshavunjika kwa mujibu wa sheria.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kushika cheo cha Naibu Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1993 hadi 1994, pamoja na nyadhifa mbalimbali za uwaziri nchini ikiwamo Mwenyekiti wa Chama cha TLP, alifunga ndoa hiyo baada ya mke wake wa kwanza, Rose kufariki dunia tarehe 21 Septemba 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!