Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Miaka 61 ya uhuru: Walilia maendeleo, uhuru na haki
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Miaka 61 ya uhuru: Walilia maendeleo, uhuru na haki

Dk. Benson Bagonza
Spread the love

WAKATI Tanzania Bara ikitimiza miaka 61 ya uhuru, Serikali imetakiwa kuhakikisha maendeleo, uhuru na haki za Watanzania zinaimarika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa katika nyakati tofati na baadhi ya Watanzania, leo Ijumaa, tarehe 9 Desemba 2022, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, amesema anamuombea kwa Mungu Rais Samia Suluhu Hassan, ili ampe nguvu za kukata minyororo yote inayopunguza haki na uhuru wa watu.

“Ninamtakia afya njema Rais SSH. Mungu amjalie afya ya mikono kushika mkasi kila wakati na kukata minyororo yote inayopunguza HAKI na UHURU wa watu. Uhuru kwanza, Maendeleo ya vitu wananchi watajitafutia wakiwa huru na kutendewa haki,” amesema Dk. Bagonza na kuongeza:

“Uhuru ni haki ya msingi isiyoondolewa na wingi au uchache wa watu. Kila mtu aone aibu kuwa baada ya miaka 61 ya uhuru, eti bado watanzania wanalazimika kuomba ruhusa ili wakutanike kuzungumza juu ya maisha yao!”

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amesema kukosekana kwa uhuru wa watu kunaathiri maendeleo ya taifa na kuwataka Watanzania kuwa wamoja katika kuwezesha mabadiliko ya mageuzi ya kimfumo, kitaasisi na kiuongozi.

“ Hakuna kilichobadilika, bado hakuna uhuru na haki ya kufanya mikutano ya hadhara, bado hakuna uhuru na haki ya kuwa na katiba mpya, bado hakuna uhuru na haki ya kuwa na tume huru ya uchaguzi, bado hakuna uhuru na haki ya kuwa taasisi imara, bado hakuna uhuru na haki juu ya haki za watu,” amesema Mnyika na kuongeza:

“Matokeo yake kiwango cha maendeleo yetu ya kiuchumi na kijamii hakilingani na umri wa taifa na kiwango cha rasilimali ambacho Mwenyezi Mungu amejalia nchi yetu yote yakiwa ni madhara ya uongozi mbovu. Hivyo, ni lazima wananchi kuwa na umoja na kuongeza kasi ya ushiriki kwenye kuwezesha mabadiliko na mageuzi ya kimfumo, kitaasisi na kiuongozi nchini.”

Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA), Sharifa Suleiman, ameiomba Serikali ihakikishe Watanzania wanakuwa huru, kama ilivyokuwa malengo ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ya kudai uhuru wa Tanganyika.

“Tunapozungumzia miaka 61 ya uhuru wa Tanzania, siwezi kusema imepiga hatua kwa sababu bado uhuru haujapatikana. Wamiliki wa uhuru ni wananchi lakini uhuru bado ni bandia . Bado Serikali inatakiwa ijitathimini kuweza kulingania uhuru wa Watanzania kama malengo na madhumuni ya kuimarisha uhuru wa Tanzania,” amesema Sharifa.

Aidha, Sharifa ameishauri Serikali Serikali kuimarisha haki za kisiasa na kijamii, ikiwa pamoja na kuondoa zuio la mikutano ya hadhara.

“Haki za binadamu bado haziko sawa hususan katika masuala mazima ya kisiasa, kuna zuio haramu linaloendelea la kutoruhusu vyama vya vya siasa vya upinzani kuweza kufanya mikutano ukizingatia hii ni haki ya msingi ya kikatiba. Wito wangu mikutano hii iachiliwe,” amesema Sharifa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!