Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mhariri Raia Mwema apata pigo
Habari Mchanganyiko

Mhariri Raia Mwema apata pigo

Martin Malera
Spread the love

 

MHARIRI wa Gazeti la Raia Mwema, Martin Malera, amepata pigo baada ya kufiwa na mkewe, Patricia Malera, ikiwa ni miezi michache tangu aondokewe na wazazi wake wote. Anaripoti Eliabu Kanyika, DSJ … (endelea).

Msemaji wa familia Clatus Mgendela, amesema kifo cha Patricia kilitokea tarehe 1 Aprili 2023 katika hospitali ya Mloganzila baada ya kuugua ghafla ya kufikishwa katika hospitali hiyo.

“Marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo, alikuwa akipata tiba katika hospitali ya Muhimbili na zingine. Hakuwa katika hali mbaya wala hajawahi kulazwa,” amesema Mgendela.

Marehemu Patricia amecha mgane na watoto watatu ambao Winifrida, Wilfred na Reginald.

Kuhusu mazishi Mgendela amesema maziko yanatarajiwa kufanyika Jumatano tarehe 5 Aprili, 2023 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam saa 9 jioni.

Amesema mwili wa marehemu utalazwa nyumbani kwake leo Jumanne tarehe 4 Aprili 2023 na kabla ya maziko kesho Jumatano kutakuwa na ibada maalum itakayofanyika katika Kanisa Katoliki la Yohane Paulo lililopo Mbezi Msakuzi.

Itakumbukwa tarehe 24 Disemba 2023, mhariri huyo alifiwa na mama yake mzazi, Amandina Sangusangu aliyefariki dunia katika Hospitali ya Ulanga Mkoani Morogoro.

Aidha tarehe 9 Februari 2023, Martin alifiwa na baba yake mzazi Fabian Malera aliyepoteza maisha katika hospitali hiyohiyo ya Ulanga.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Moduli ya kuwasilisha rufaa za zabuni kieletroniki kuanza Julai

Spread the loveMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mshindi ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ akabidhiwa trekta

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imehitimisha msimu wa tatu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hati Fungani ya NMB Jamii yaanza kuuzwa Soko la Hisa London

Spread the loveBenki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

error: Content is protected !!