Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TRA yakusanya Tril. 5.9/- kuanzia Januari hadi Machi
Habari Mchanganyiko

TRA yakusanya Tril. 5.9/- kuanzia Januari hadi Machi

Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA
Spread the love

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA), imekusanya Sh. 5.9 trilioni katika robo ya tatu (Januari-Machi) ya mwaka wa fedha 2022/23 ikiwa ni sawa na asilimia 97.9 ya lengo la kukusanya Sh. 6.0 trilioni katika kipindi hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 4 Aprili 2023 na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata katika taarifa yake kwa umma kuhusu mwenendo wa makusanyo.

Amesema makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.1 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Ametaja sababu zilizosaidia ongezeko hilo kuwa ni uboreshaji wa mfumo w aukusanyaji kodi ambayo imerahisisha utaratibu wa ulipaji kodi kwa hiari.

Pia ametaja sababu nyingine ni kuongezeka kwa uwezo wa walipakodi katika kulipa malimbikizi ya kodi kutokana na Serikali kongeza kasi ya ulipaji wa marejesho ya kodi.

Aidha amesema kuimarika kwa mahusino baina ya Mamlaka na walipakodi ikiwemo utatuzi wa migogoro ya kodi ya nje ya mahakama pamoja na kushughulikia malalamiko ya kodi kwa wakati, ni sababu nyingine ya ongezeko hilo.

Vilevile amesema kujengeka kwa imani kwa wafanyabiashara kufuatia uwezeshaji wa mazingira mazuri ya biashara nchini, kumeshangia kwa kiasi kikubwa ongezeko hilo.

“Kwa niaba ya Menejimengi ya TRA napenda kutoa shukrani za dhati kwa walipakodi na wadau mbalimbali kwa kutuwezesha kufikia ufanisi huu,” amesema Kidata.

Ametoa rai kwa wananchi wote kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa ktimiza wajibu wao wa kisheria ikiwmeo kuwasilisha ritani kwa wakati, kuzuia na kulipa kodi ya zuio na kulipa kodi zote stahiki.

Pia amesema ni wajibu wa kila mwananchi anaponunua bidhaa kudai risiti ya kielekroniki ya EFD yenye thamani sahihi ya kiasi alicholipa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!