Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yamwaga mamilioni halmashauri tatu Morogoro
Habari Mchanganyiko

NMB yamwaga mamilioni halmashauri tatu Morogoro

Spread the love

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika sekta ya afya na elimu kwa halmashauri tatu za Mlimba, Malinyi na Manispaa ya Morogoro ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha faida kwa jamii baada ya mwaka 2022 kupata faida ya kiasi cha Sh429 bilioni huku ikitenga kiasi cha Sh6.2bilioni kwa ajili ya kuhudumia jamii katika miradi ya maendeleo kwa mwaka huu hapa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza katika shule ya sekondari Chita halmashauri ya wilaya ya Mlimba, Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kati, Nsolo Mlozi alisema benki hiyo kila mwaka imekuwa ikitenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kurejesha faida kwa jamii katika kutoa misaada sekta za afya, elimu na majanga ya asili yanayojitokeza na mwaka huu imetenga kiasi cha Sh6.2 bilioni.

Mkuu wa wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba kushoto na Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kati, Nsolo Mlozi wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya msingi Mwembeni baada ya benki hiyo kutoa msaada wa meza, viti, madawati na vifaa vya afya vyenye thamani ya sh42.3milioni baada ya benki hiyo kutoa msaada wa meza, viti, madawati na vifaa vya afya vyenye thamani ya sh42.3milioni kwa Manispaa ya Morogoro, Malinyi na Mlimba mkoani hapa.

Nsolo alisema kwa mwezi Machi mkoa wa Morogoro imenufaika na misaada katika sekta ya elimu na afya kwa kupata vifaa katika sekta hizo vikiwa na thamani ya Sh42.3milioni katika halmashauri tatu za Manispaa ya Morogoro, Malinyi na Mlimba.

“Leo (jana) NMB kwa mwezi Machi tumetoa vifaa katika sekta ya elimu na afya kama sehemu yetu ya kuunga mkono serikali miradi ya maendeleo baada ya sisi kupata faida na mwaka ulioisha tumeweza kupata faida ya Sh429 bilioni na mwaka huu benki imeongeza fedha kwenda kwa jamii kutoka kiasi cha sh4bilioni hadi kufikia kiasi cha sh6.2bilioni hii ni kwa ajili ya kuhudumia jamii katika miradi ya maendeleo hapa nchini tukiwa na utamaduni wetu wa kurejesha faida kwa jamii,” alisema Nsolo.

Meneja Mahusiano Huduma kwa Serikali Benki ya NMB, Peter Massawe ametaja vifaa hivyo ni chuo cha Bigwa viti 100 na meza 100, shule ya msingi Sinyaulima Ngerengere vifaa vya ujenzi, Chita sekondari viti 50 na meza 50, Ngoheranga vita 50 na meza 50, shule ya msingi Mwembeni Malinyi madawati 50 na Hospitali ya wilaya Malinyi ikipokea vitanda nane vya kujifungulia akinamama wajawazito.

“Vifaa tulivyokabidhi vina thamani ya Sh42.3 milioni katika halmashauri tatu za Manispaa ya Morogoro, Malinyi na Mlimba katika sekta ya elimu na afya lakini Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa ni miongoni mwa waliopata viti 100 na mezo 100 kwa ajili ya kupunguza changamoto kwa wanafunzi na shule za msingi na sekondari ambavyo wamepata viti, meza na madawati,” alisema Massawe.

Mkuu wa wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba (wa pili kushoto), akipokea vifaa tiba mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kati, Nsolo Mlozi (wa tatu kulia) katilka hafla ya makabidhiano ya vitanda nane vy kujifungukia na mashuka 60 kwa Hopsitali hya wilaya ya Malinyi. Benki ya NMB imetoa msaada wa jumla ya thamani hya shilingi 42.3 milioni kwa halmashauri tatu za Morogoro, Mlimba na Malinyi zote za Mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi, Mhe. Pius Mwelase na kulia ni meneja wa mahusiano ya Benki ya NMB na serikali kwa kanda ya Kati, Peter Masawe na wapili kulia ni meneja wa Benki ya NMB Tawi la Malinyi, Omari Hamisi

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba alisema benki hiyo imekuwa msaada kwa serikali katika kutoa msaada sekta ya afya, elimu kutokana na kuipunguzia mzigo katika kutoa vifaa katika sekta hizo na kuomba taasisi nyingine za kifedha kuiga mfano kwa NMB kurejesha faida wanazopata kwenda katika jamii.

Kaimu Kurugenzi halmashauri ya wilaya ya Mlimba, Wakili Kulaba Dotto alisema baada ya benki hiyo kutoa misaada hiyo kwa shule za sekondari ya Chita na msingi Kalengakeru bado kuna upungufu wa meza na viti kwa shule za sekondari 1690.

“Viti 50 na meza 50 tulivyovipokea na madawati vitasaidia kupunguza upungufu kwa wanafunzi wetu kabiliana na na changamoto ya uhaba wa meza, viti na madawati katika shule zetu za msingi na sekondari na kwa sasa sekondari pekee kuna upungufu wa meza na viti 1690 kwa shule 31 ambazo zina wanafunzi 15,890 na meza na viti vilivyopo ni 14,200 hivyo tunaweza kuona kuna kila sababu ya kuhitaji msaada zaidi ili watoto wasome katika mazingira tulivu zaidi,” alisema Wakili Kulaba.

2 Comments

  • (i) Ubaguzi wa rangi na ubaguzi dhidi ya watoto kwa misingi ya makabila, lugha na dini umeenea duniani na kuleta athari kwenye mfumo wa haki, usawa na hata KUJISOMEA, limesema Shirika la UN la UNICEF.
    (ii) South Sudan’s refugee crisis remains the largest in Africa. Those displaced within and from South Sudan jointly call for an end to the conflict for a chance to return to a peaceful home.
    (iii) UNHCR’s support for ~1 million Rohingya refugees in Bangladesh is underfunded. Critical services such as health, housing, water, sanitation and hygiene are at risk.
    (iv) On average, over 40 million people have been estimated to be food insecure every year by the SADC Regional Vulnerability Assessment Programme over the past five years.
    (v) Balaaa NA NI HATARI: Wagandana wakifanya mapenzi, aliewanasisha aeleza alivyofanya, mganga atoa masharti mazito.
    (vi) Wamiliki wa ardhi katika kata ya Mabwepande Wilaya ya Kindondoni jijini Dar es Salaam wameililia serikali wakitaka kuondolewa kwa wavamizi wa ardhi eneo hilo wanaodaiwa kuhatarisha usalama.
    (vii) Americans watched in horror as the terrorist attacks of Sept. 11, 2001, left nearly 3,000 people dead in New York City, Washington, D.C., and Shanksville, Pennsylvania.
    (viii) Mwalimu alikuwa anafundisha shule ya vichaa na alijiwekea utaratibu kuwa kila mwisho wa mwaka atawapa jaribio nani amejaribu kupona ukichaa siku moja alipokuwa darasani alichora mlango ubaoni.
    (ix) Utafiti mkubwa uliofanywa duniani na kuchapishwa katika jarida la lancet umethibitisha kwamba utafiti uliofanywa awali na kuonyesha kwamba hakuna usalama katika unywaji wa pombe.
    (x) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994 hayakuwa ya bahati mbaya wala yasiyoweza kuepukika.

  • (i) Dissertation (Confession Time):- Do high Unemployment Rate Influence Someone other Guys Creativity in solving PROBLEM, PRIDE, SOCIAL STATUS, WEALTH and Planning (TITANIC SOLVERS IN PARLIAMENT)?!

    (ii) Ubaguzi wa rangi na ubaguzi dhidi ya watoto kwa misingi ya makabila, lugha na dini umeenea duniani na kuleta athari kwenye mfumo wa haki, usawa na hata KUJISOMEA, limesema Shirika la UN la UNICEF.
    (iii) South Sudan’s refugee crisis remains the largest in Africa. Those displaced within and from South Sudan jointly call for an end to the /conflict for a chance to return to a peaceful home.
    (iv) UNHCR’s support for ~1 million Rohingya refugees in Bangladesh is underfunded. Critical services such as health, housing, water, sanitation and hygiene are at risk.
    (v) On average, over 40 million people have been estimated to be food insecure every year by the SADC Regional Vulnerability Assessment Programme over the past five years.
    (vi) Balaaa NA NI HATARI: Wagandana wakifanya mapenzi, aliewanasisha aeleza alivyofanya, mganga atoa masharti mazito.
    (vii) Wamiliki wa ardhi katika kata ya Mabwepande Wilaya ya Kindondoni jijini Dar es Salaam wameililia serikali wakitaka kuondolewa kwa wavamizi wa ardhi eneo hilo wanaodaiwa kuhatarisha usalama.
    (viii) Americans watched in horror as the terrorist attacks of Sept. 11, 2001, left nearly 3,000 people dead in New York City, Washington, D.C., and Shanksville, Pennsylvania.
    (ix) Mwalimu alikuwa anafundisha shule ya vichaa na alijiwekea utaratibu kuwa kila mwisho wa mwaka atawapa jaribio nani amejaribu kupona ukichaa siku moja alipokuwa darasani alichora mlango ubaoni.
    (x) Utafiti mkubwa uliofanywa duniani na kuchapishwa katika jarida la lancet umethibitisha kwamba utafiti uliofanywa awali na kuonyesha kwamba hakuna usalama katika unywaji wa pombe.
    (xi) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994 hayakuwa ya bahati mbaya wala yasiyoweza kuepukika.
    (xii) Mhe. WAZIRI Mkuu baada ya SERIKALI KUHAMIA DODOMA LINI VYOMBO VYA HABARI VYA ITV, EATV, TBC, AZAM TV, WASAFI TV, MWANANCHI VITAHAMIA DODOMA KWA LAZIMA.(TULIBUNI DSM HATUWEZI KUBUNI DODOMA) SWAHILI
    (xiii) Tangazo:- Tunauza Dawa za kufupisha urefu wa mwandamu (kama ni mrefu NA UNATAKIWA KUWA MFUPI HUDUMA ndani ya siku 3) lengo ni kiongozi mkubwa Duniani kama ni Mrefu Ukubarike kwa asilimia 100%

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Moduli ya kuwasilisha rufaa za zabuni kieletroniki kuanza Julai

Spread the loveMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mshindi ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ akabidhiwa trekta

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imehitimisha msimu wa tatu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hati Fungani ya NMB Jamii yaanza kuuzwa Soko la Hisa London

Spread the loveBenki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

error: Content is protected !!