Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO
Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, amalize changamoto ya mgawo wa umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo leo tarehe 26 Septemba 2023, Ikulu jijini Dar es Salaam, akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua tarehe 23 Septemba mwaka huu, akiwemo Mhandisi Nyamo-Hanga.

Rais Samia amesema tatizo la umeme ni janga kwa taifa, huku akisema miongoni mwa sababu zake ni uchakavu wa mitambo ambapo amemtaka Mhandisi Nyamo-Hanga, kusimamia marekebisho yake.

“Nyamo-Hanga unakwenda TANESCO nikijua kwamba wewe sio Mgeni TANESCO, unaijua vizuri TANESCO kwahiyo utakwenda pale kuongeza pale Maharage alipofikia, tuna crisis, crisis ile ni crisis yetu kama taifa sio ya mtu, maana mtu mwingine anaweza kusema Maharage kisa kukatikakatika umeme kaondoshwa hapana, mitambo ile kwa muda mrefu haikufanyiwa service sasa tunakwenda kuifanyia service kwa pamoja,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Kwa hiyo kuna upungufu wa umeme, najua utaweza. Nakupa miezi sita nakuangalia pale TANESCO, kazi yako ya kwanza ni kusimamia ukarabati wa hiyo mitambo. Lakini baada ya hiyo miezi sita, nisisikie tena kelele za kukatika kwa umeme, tutasaidiana lakini nenda ninajua utaweza.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!